Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kanuni ya Hukumu

  Sheria ya Mungu ndiyo kanuni au kipimo katika hukumu “Mche Mungu, na uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu” “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi” “Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru”. Mhubiri 12:13-14; Yakobo 2:12.TU 233.3

  Wale watakaohesabiwa kuwa wanastahili, watakuwa na sehemu katika ufufuo wa wenye haki. Yesu alisema “Wale wahesabiwao kuwa wanastahili kuupata ulimwengu ule na kufufuka katika wafu …. Nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo” “Wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima”. Luka 20:35-36; Yohana 5:29. Wafu, ambao ni wenye haki hawafufuki mpaka hukumu ambayo imewahesabu kuwa wanastahili “ufufuo na uzima” imalizike Hivyo hawatakuwako katika hukumu hiyo, wakati mambo yao yanapoamuliwa.TU 233.4

  Yesu ndiye atakuwa mtetezi wao mbele za Mungu “Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki”. “Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndiyo mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu” “Naye kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee” 1Yoh. 2:1 Waebrania 7:25; 9:24.TU 234.1

  Vitabu vinapofunguliwa katika hukumu, maisha ya watu wote waliomwamini Yesu yanachunguzwa mbele za Mungu. Wakianzia na watu wa kwanza kabisa kuishi ulimwenguni. Mtetezi wetu analeta habari za wote wa kila kizazi. Majina mengine yanakubalika, na mengine yanakataliwa, maana kila jina linatajwa na habari zake zinachunguzwa barabara. Mtu ye yote akionekana kuwa dhambi zake bado ziko kitabuni, wala hajaziungama ili zifutwe, naye asamehewe, jina lake hufutwa katika kitabu cha uzima. Bwana alimwambia Musa, “Yeyote aliyetenda dhambi ndiye nitamfuta katika kitabu changu” Kutoka 32:33.TU 234.2

  Watu wote ambao wametubu kwa kweli na kwa imani wamedai damu ya Kristo kuwa ukombozi wao, wamesamehewa, na majina yao yameandikwa mbinguni. Kwa jinsi walivyokuwa washiriki wa haki ya Kristo, na tabia zao zimeonekana kuwa zinaafikiana na tabia ya Kristo na sheria ya Mungu, dhambi zao hufutwa, na wao watahesabiwa kuwa wanastahili kupata uzima wa milele. Bwana asema “Mimi naam mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe; wala sitazikumbuka dhambi zako” “Yeye ashindaye atavikwa mavazi meupe…. Nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele za malaika zake” Basi, kila mtu atakayenikiri mbele za watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Isaya 43:25; Ufunuo 3:5; Mathayo 10:32-33.TU 234.3

  “Yesu mtetezi atetea wote walioamini damu yake ili awapeleke katika makao ya Edeni, akiwafanya washiriki katika urithi na utawala wake na katika mamlaka ya kwanza” Mika 4:8. Sasa Kristo ataka hali ya mpango wa kwanza wa uumbaji, irudishe, na kuwafanya watu hawa kana kwamba hakufanya dhambi. Anaomba kwamba watu wake wasisamehewe na kupewa haki peke yake bali wawe washiriki katika utukufu wake, na waketi katika kiti chake cha enzi.TU 234.4

  Wakati Yesu anaomba kwa ajili ya raia zake wa neema, shetani anawashitaki mbele za Mungu. Anataja habari za maisha yao ya nyuma, anataja tabia zao mbaya, walivyokuwa wabovu wasifanane na Kristo, anaonyesha dhambi zao zote, ambazo aliwashawishi wakafanya. Kwa hiyo anadai kuwa ni watu wake wenye dhambi kama yeye.TU 235.1

  Yesu hatetei dhambi zao, bali huonyesha toba zao na imani yao. Anadai kuwa wasamehewe kwa ajili ya toba walivyotubu. Anainua mikono yake iliyopigwa na misumari, mbele za Baba, akisema “nimewachora katika viganja vyangu. Dhabihu za Bwana ni roho iliyovunjika. Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee, Mungu, hutaudharau”. Zab. 51:17.TU 235.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents