Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kufutwa Kabisa kwa Dhambi

  Kazi ya hukumu ya upelelezi na ya kufutwa dhambi itakamilika kabla ya kurudi kwake Yesu duniani. Katika mfano wa hema takatifu, kuhani alitoka na kuwabariki watu wa mkutano siku ya upatanisho. Vivyo hivyo na Kristo pia, baada ya kazi yake ya uombezi, atatokea bila “dhambi kwa hawa wamtazamao kwa wokovu” Waebrania 9:28.TU 235.5

  Kuhani alipokuwa akizihamisha dhambi kutoka katika patakatifu aliziungama na kuziweka juu ya mbuzi wa Azazeli. Kristo naye ataweka dhambi zote juu ya Shetani ambaye ndiye mwanzilishi wa dhambi. Mbuzi wa Azazeli alikuwa akipelekwa porini Mambo ya Walawi 16:22. Shetani naye akichukua dhambi alizosababisha na kuwashawishi watu wa Mungu kufanya, atafungwa maabusu muda wa miaka elfu moja, katika nchi iliyoharibika na kubomoka, baadaye ataadhibiwa katika ziwa la moto ambao utawatetekeza waovu. Hivyo basi mpango wa wokovu utafikia ukamilifu wake, wakati dhambi itakapokuwa imeharibiwa kabisa kabisa.TU 235.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents