Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ubinafsi wa Siri Wadhihirika

  Ubinafsi wa kisirisiri huwa wazi kabisa katika vitabu vya mbinguni. Mara ngapi watu humpa shetani nyakati zao, mawazo yao na nguvu zao ambazo ni mali ya Mungu. Wanaojidai kuwa wafuasi wa Kristo, wanajitumbukiza katika kutafuta mali ya dunia, au katika anasa za dunia. Fedha, wakati na nguvu hutumiwa katika mambo ya kujinufaisha na kutukuza ubinafsi. Muda wa kutumiwa katika maombi ni kidogo sana, na muda wa kuchunguza Maandiko na kuungama dhambi ni kidogo sana.TU 236.3

  Shetani amevumbua mambo mengi mno ya kutushughulisha. Mdanganyifu mkuu huyu, anachukia ukweli ambao hutuelekeza kwa Mkombozi wetu anayetuombea. Mambo yake yote hutoa mawazo ya watu yasimfikiri Kristo na uombezi wake.TU 236.4

  Watu ambao wanataka kufaidi uombezi wa Kristo, inawapasa wasiruhusu kitu cho chote kiwazuie kutimiza wajibu wao unaopasa wokovu wao mbele za Mungu. Nyakati zao za thamani, lazima zitumike katika kuomba na kujifunza neno la Mungu, badala ya kujifurahisha na kufukuzana na uchumi wa nchini. Patakatifu pa mbinguni na kazi ya uchunguzi wa hukumu huko mbinguni vingekuwa dhahiri katika mawazo yao daima. Wote wanahitaji kuielewa barabara kazi ya kuhani wao Mkuu, uombezi wake kwa ajili yao. Au la, sivyo watashidwa kuelewana naye katika shughuli anayowashughulikia.TU 237.1

  Patakatifu pa mbinguni ndipo kiini cha kazi Kristo anayowashughulikia wanadamu. Kazi hiyo inamhusu kila mtu aliyeko duniani. Inadhihirisha mpango wa wokovu, inatuleta mpaka kwenye mashindano makuu baina ya haki na uovu.TU 237.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents