Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  4/ Waldenses Waitetea Imani

  Katika muda mrefu wa utawala wa upapa, kulikuwako na mashahidi wa Mungu waliothamini Imani katika Kristo kwamba ndiye Mwombezi na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Walishikilia mwongozo wa Biblia kuwa ndio kiongozi maishani, na kuitukuza Sabato ya kweli. Walidhihakiwa na kuitwa wazushi, maandiko waliyoandika yakapigwa marufuku na kuelezwa vibaya au kuharibiwa lakini walisimama imara tu.TU 21.1

  Hawajulikani sana, isipokuwa mabarazani walikoshtakiwa. Walionekana kana kwamba ni wazushi, Rumi ilikusudia kuwaharibu wao au maandishi yao. Rumi pia ilijitahidi kuharibu kumbukumbu zote za mambo yao ya ukatili walivyowatendea wapinzani wao, yaani wale ambao hawakukubaliana na mafundisho yao. Kabla mashine za kuchapa vitabu hazijagunduliwa, vitabu vilikuwa vichache sana, kwa hiyo Warumi waliweza kuviharibu kwa urahisi na kuvimaliza. Muda si mrefu Papa alipata uwezo akafaulu kuwafuatilia mbali wale waliompinga.TU 21.2

  Katika Uingereza ukristo uliingia na kustawi zamani sana, ambao haukupotoshwa na uasi wa Rumi. Mateso yaliletwa na watawala wakafiri, ndicho kitu kilichowapata huko England, walipata hifadhi huko Scotland. Na hivyo ukweli ukafika Ireland. Ukweli huo ulipokea kwa furaha na wenyeji wa nchi hizo.TU 21.3

  Wakati watu wa Saxon walipovamia Uingereza, ukafiri ulipata nafasi ya kustawi huko, na hivyo wakristo walifukuziwa sehemu zilizo mbali. Kutoka Ireland alikuja Kolumba na wenzake ambao walifanya kazi yao na kuishi katika kisiwa cha Iona. Kati ya wahubiri hao alikuwamo mshika Sabato ya Biblia, na kwa hiyo Sabato ilijulishwa kwa watu. Shule ilianzishwa huko Iona, ambayo iliwatayarisha wahubiri waliokwenda Scotland, Uingereza, Ujerumani na Uswisi na hata Italia.TU 21.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents