Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ukweli Hutakasa

  Mdanganyifu mkuu anazo hila nyingi sana alizoandaa ili kuwapotosha watu wa aina mbalimbali ambao atawapata. Ni nia yake kuingiza watu kanisani ambao sio waongofu ili alete mashaka na hali ya kutoamini kwa wakristo kwa ajili ya hao. Watu ambao hawana imani kwa Mungu huingia na kushika kanuni kanisani na kuhesabiwa kuwa ni wakristo, kwa hiyo huingiza mambo ya kikafiri kanisani, na kuhesabiwa kuwa ni sehemu ya ukristo. Shetani anajua kuwa ukweli ukipokelewa kamili mioyoni hutakasa maisha. Kwa hiyo hutafuta kuingiza mafundisho ya uongo yahesabike kuwa ni sehemu ya Injili. Tangu mwanzo watumishi wa Mungu walikuwa wakishindana na waalimu wa uongo sio kuwa ni watu wabaya tu, bali ni waangamizaji halisi. Eliya, Yeremia, Paulo waliwapinga vikali watu ambao waligeuka upande, wakaacha neno la Mungu na kufundisha mambo mengine. Hivyo wenye imani potofu ambao wanauhafifisha ukweli wa Biblia na imani ya kweli, hawakukubaliwa na watumishi hawa wa Mungu ambao walikuwa watetea kweli.TU 254.1

  Maelezo hafifu na mapotofu ya Maandiko Matakatifu na imani potofu katika makanisa ya ulimwengu ambayo huleta mapingano na mafarakano, ni kazi ya mdanganyaji mkuu ili kupotosha mawazo ya watu. Mafarakano na tofauti katika makanisa ni matokeo ya kuacha ukweli wa maandiko Matakatifu, ili kuunga mkono nia zao.TU 254.2

  Uli kusudi wapate uthibitisho wa nia zao, wengine husoma sehemu ya maandiko wakidhani kuwa inawaunga mkono ambavyo fungu zima la maandiko huwapinga. Kwa ujanja wa yule joka huyatengeneza yapate kufaa kwa njia potofu yadhaniwe kuwa yamo katika ukweli. Wengine hutafsiri mifano na vielelezo kwa upande wao, wala hawajali ukweli wote wa maandiko. Kisha huleta makosa yao ya kuieleza Biblia vibaya kuwa ndiyo ukweli wa Biblia.TU 254.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents