Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Makosa ya hatari

  Baadhi ya makosa ya hatari ambayo Mwovu hutumia kwa ufanisi zaidi ni ishara za uongo za kuongea na wafu. Watu wanapokataa ukweli huangukia ndani ya madanganyo.TU 256.1

  Kosa jingine ni kule kukana Uungu wa Kristo, wakisema kuwa kabla ya kuzaliwa hapa duniani, hakuwako kamwe. Jambo hili hupingana na elezo lake mwenyewe linalozungumza juu ya uhusiano wake na Baba yake kabla ya kuja hapa duniani. Fundisho hili huharibu ukweli wa Biblia kuhusu uhusiano huo. Iwapo watu wanakanusha ushahidi wa Biblia kuhusu Uungu wa Kristo, ni kazi bure kubishana nao. Hakuna hoja itakayowaamisha. Mwenye kushikilia mambo hayo hawezi kufahamu habari za Kristo, wala mpango wa Mungu wa wokovu wa Biblia.TU 256.2

  Kosa jingine ni kule kukanusha kuwa shetani siye kiumbe kamili chenye utu na nafsi. Husema kwamba jina hilo hutumika kuonyesha mawazo ya watu waovu na tamaa zao ovu.TU 256.3

  Kosa jingine ni lile lifundishwalo kwamba kuja kwa Kristo mara ya pili ni kule kunakotukia mtu afapo. Fundisho hilo hupotosha ukweli wa Biblia kuhusu kuja kwake katika mawingu ya mbinguni. Shetani amekuwa akiwaambia watu kuwa, “Tazameni yuko sirini” Mathayo 24:23-26. Na wengi wamepotea kwa kuamini uongo huo.TU 256.4

  Tena wanasayansi husema kuwa hakuna jawabu la kweli katika maombi. Hilo ni uvunjaji wa sheria ya kawaida ya miujiza, na miujiza haipo. Husema kuwa ulimwengu hutawaliwa na sheria za asili, ambazo Mungu hahusiki nazo. Hivyo huonyesha kwamba Mungu pia hutawaliwa na sheria hizo, kana kwamba yeye hana la kufanya na sheria hizo. Je, Kristo na wanafunzi wake hawakufanya miujiza? Kristo yule yule yu tayari kusikiliza sala za watu wake, sawasawa na wakati ule alipokuwa akiishi kati yao. Ni mpango wa Mungu kwetu kujibu maombi yetu, na kutenda maajabu, ambayo kama tusingemwomba, yasingelitendeka.TU 256.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents