Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uwongo Mkuu

  Aliyewaahidi watu uzima kwa kutotii sheria, alikuwa mwongo mkuu, na mdanganyaji mkuu. Akizungumza kwa njia ya nyoka huko Edeni, alisema, “Hamtakufa hakika”. Hilo lilikuwa tangazo lake la kwanza kuhusu kutokufa kwa roho. Walakini tangazo hili ambalo ni uwongo wa Shetnai ni mwangwi unaohubiriwa na wahubiri wengi, na hupokelewa na watu maelfu, sawa kama vile lilivyopokelewa na wazazi wetu wa kwanza. Tangazo la Mungu ni hili “Roho itendayo dhambi itakufa (Eze. 18:20) lakini Shetani akageuza kuwa, maana yake ni roho itendayo dhambi haitakufa. Kama mtu ageruhusiwa kutwaa matunda ya mti wa uzima baada ya kukosa, dhambi ingedumishwa milele. Lakini hakuna hata mmoja wa wazao wa Adamu aliyeruhusiwa kula matunda ya uzima. Kwa hiyo hakuna mwenye dhambi ambaye hudumu milele.TU 261.1

  Baada ya anguko la mwanadamu, shetani aliwaagiza malaika zake wawafundishe wanadamu waamini kuhusu umilele wa roho, kwamba hata kama mtu amekufa, roho yake huendelea kuishi. Baada ya kuwaaminisha watu namna hiyo, huwaongoza waamini kwamba mtu mbaya afapo huendelea kuteseka katika uharibifu milele. Sasa mwovu huyu hutupa lawama kwa Mungu kwamba huwaadhibu wote ambao hawampendezi, na ya kwamba wakati wanapoteseka motoni namna hii, Mungu huwachungulia na kutosheka. Hivyo ndivyo mwovu anavyompaka Mwumbaji matope. Ukatili ni wa shetani. Mungu ni Upendo. Shetani ndiye huwashawishi watu kufanya dhambi na kuwaharibu ikiwa anaweza. Shetani hupindua mafundisho kuhusu upendo, rehema, haki, yakaonekana kuwa machukizo ya ukatili wa kutesa watu katika moto huko ahera milele na milele.TU 261.2

  Je, katika Neno la Mungu mafundisho ya jinsi hiyo yanapatikana wapi? Hali ya kawaida ya kujisikia kwa kibinadamu ndiyo ilinganishwe na ukatili wa kishetani? La, Neno la Mungu halifundishi namna hiyo “Kama mimi niishivyo, asema Bwana Mungu, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu na kuiacha njia yake mbaya, akaishi, ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa?” Eze. 33:11.TU 261.3

  Je, Mungu hupendezwa kuona mateso ambayo hayana mwisho ya watu wake? Je, hufurahia kuona viumbe wake wakiomboleza siku zote katika moto anaowachoma? Je, vilio hivyo vya huzuni vinakuwa nyimbo tamu za kusikilizwa na Mungu Mwenyenzi mwenye pendo? Hayo ni makufuru na matusi kwa Mungu. Utukufu wa Mungu hauongezwi na kustawishwa kwa mateso ya dhambi milele na milele.TU 262.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents