Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uzushi Kuhusu Mateso ya Milele.

  Mwovu ameleta uzushi wa mafundisho kuhusu mateso ya milele. Dini ya Biblia yenye kujaa pendo na wema wa kila hali, imetiwa giza na kufunikwa na hali ya hofu na ushirikina. Shetani amechafua tabia ya Mungu kwa kumsingizia mambo ya kila namna. Mwumbaji wetu mwenye rehema anahesabiwa kana kwamba ni mkatili mwenye kuogopwa kwa hofu na kutetemeka kiasi cha kuchukiwa. Hali ya kutisha ya tabia ya Mungu imeelezwa ulimwenguni pote na wahubiri, hata imewafanya watu mamilioni kuwa watu wenye mashaka kwa Mungu na wakafiri.TU 262.2

  Fundisho la mateso ya milele ni moja ya mafundisho mapotofu, mvinyo ya makufuru (Ufunuo 14:8; 17:21) ambayo Babeli imewalevya mataifa yote. Wajumbe wa Kristo wameyapokea mafundisho haya kutoka kwa Rumi, kwa vile walivyokubali kuipokea sabato bandia, ambayo ni siku ya jumapili. Tunapoliacha neno la Mungu na kugeukia mafundisho ya uwongo kwa ajili ya mapokeo kutoka kwa baba zetu, pale tunatumbukia katika hukumu iliyotangazwa juu ya Babeli; yaani tunakunywa mvinyo wa uasherati wake.TU 262.3

  Watu wengi wamevutwa kusimama upande mpotovu. Wao huona jinsi Biblia inavyomwonyesha Mungu kwamba ni Baba mwenye huruma na upendo hawawezi kukubali kuwa hawezi kuwatia viumbe wake katika hali ya kuwa matesoni milele na milele. Wakiamini kuwa roho za binadamu hazifi kamwe; na tena kwamba watu wote wataokolewa. Hivyo basi mwenye dhambi anaweza kuishi katika anasa za dhambi bila kujali maagizo ya Mungu, na baadaye Mungu atampokea tu. Mafundisho ya namna hiyo husisitiza juu ya rehema za Mungu na kupuuza haki yake. Mambo kama haya huwafurahisha watu wawezao mambo ya kimwili tu.TU 262.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents