Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wokovu wa Jumla Maandiko Hayausemi.

  Watu wanaoamini kuwa uko wokovu wa jumla, hufuta maandiko ya Biblia. Wahudumu wa Kristo huukariri kariri uwongo ule nyoka aliousema katika Edeni, kwama “Hamtakufa hakika” “Siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu” alisema kuwa mdhambi mashuhuri —mwuaji, mwizi, mzinzi, baada ya kufa huingia katika raha ya milele. Jambo ambalo ni hadithi ya uwongo kabisa. Hivyo huwafurahisha wapenda anasa za ulimwengu.TU 262.5

  Kama ingalikuwa kweli kwamba watu wote huenda mbinguni moja kwa moja wakati wanapokufa, basi sote tungalitamani kifo kuliko kuishi. Wengi wameongozwa na imani ya jinsi hii. Wamejiua wenyewe ili wapate kwenda katika ulimwengu wa raha huko mbinguni kuliko kuhangaika hapa chini na maisha haya ya taabu.TU 263.1

  Mungu amesema wazi katika Neno lake kuwa atawaadhibu wote wavunjao sheria yake. Je, anazo huruma nyingi kiasi cha kuwaacha wenye dhambi bila kuwaadhibu? Hebu tazameni msalaba wa kalvari. Kifo cha Mwana wa Mungu huthibitisha kuwa, “Mshahara wa dhambi ni mauti” Warumi 6:23, kwamba kila uvunjaji wa sheria ya Mungu ni lazima upate mshahara wa namna hiyo. Kristo asiye na dhambi akafanywa kuwa dhambi kwa ajili ya wanadamu. Aliuchukia uasi na hatia ya mwanadamu, akifichwa uso wa Babaye mpaka roho yake ilipovunjika na uhai wake kutoweka kabisa, yote hayo yalitendeka ili mwanadamu akombolewe. Na kila mtu anayekataa kupokea toleo hilo lililotolewa kwa gharama kuu namna hiyo, lazima apate mshahara ambao ni malipo ya uasi wake mwenyewe. Adhabu hiyo ataibeba mwenyewe.TU 263.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents