Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Masharti Yamewekwa

  “Nami nitampa mwenye kiu chemichemi za maji ya uzima bure”. Ahadi hii ni ya wenye kitu tu “Yeye ashindaye atayarithi haya yote, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu” ufunuo 21:6-7. Masharti yamewekwa. Ili kurithi mambo yote, ni lazima tushinde dhambi, “Haitakuwa heri kwa mwovu” Mhubiri 8:13. “Mwovu anajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira ya ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake” “Dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu” Warumi 2:5-6,9.TU 263.3

  “Hakuna mwasherati wala mchafu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu” “Heri wazishikao amri zake, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya” Waefeso 5:; ufunuo 22:15.TU 263.4

  Mungu amewaonyesha wanadamu namna anavyofanya na dhambi. “Wote wasio haki atawaharibu” “Wakosaji wataangamizwa pamoja. Wasio haki mwisho wao wataharibiwa” Zab. 145:20; 37:38. Mamlaka ya Mungu yatakomesha maasi walakini malipo ya haki yatadumishwa katika tabia ya Mungu mwenye rehema na fadhili.TU 264.1

  Mungu halazimishi dhamiri ya mtu. Hana haja ya utii wa juu juu. Anataka viumbe vyake wampende kwa sababu anastahili upendo. Anataka wamtii kwa kuwa wanatambua kuwa kwa yote anayowatendea wanaona ni haki na inapasa kutoa shukrani, kwa hekima na haki na fadhili zake.TU 264.2

  Kanuni ya serikali ya Mungu inaafikiana na maneno ya Kristo, kwamba “Wapendeni adui zenu” Mathayo 5:44.TU 264.3

  Mungu huwapatiliza waovu kwa ajili ya manufaa ya wote wa ulimwengu, na hata kwa manufaa ya hao wanaopatilizwa. Angetaka kuwafanya wajisikie wenye furaha. Huwazungushia na kila aina ya upendo wake na rehema zake. Wakipokea vipaji vyake, lakini bila kujali. Daima wanapokea vipawa vyake lakini hawamtii Mungu. Bwana amevumilia muda mrefu upotovu wao lakini wakiendelea kuasi tu. Je, atawafunga kwa minyororo upande wake ili wafanye mapenzi yake?TU 264.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents