Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hawako Tayari Kuingia Mbinguni

  Wale waliomchagua Shetani kuwa kiongozi wao hawako tayari kuingia mbingui mbele za Mungu, Kiburi, udanganyifu, ufedhuli, ukatili vimekwisha kukazwa katika tabia zao. Je, wanaweza kwenda mbinguni wakaishi pamoja na wale waliowachukia walipokuwa duniani? Ukweli hautakubaliana na uwongo; unyenyekevu hauendi pamoja na majivuno; usafi wa maisha hautapatana na udhalimu; upendo usio na ubinafsi hautaafikiana na hali ya ubinafsi. Mbingu itawapa kitu gani wale waliozama katika kujipenda nafsi?TU 264.5

  Ingewezekana kwa watu ambao wanamchukia Mungu, na ukweli, na utakatifu, kuunganika na kundi la mbingu, linalopenda kuimba nyimbo za furaha na sifa?TU 264.6

  Walipata muda wa miaka mingi ya kujirekebisha, lakini hawakujishughulisha kupenda usafi wa maisha. Wala hawakujifunza lugha ya mbinguni. Sasa, wamechelewa.TU 264.7

  Muda wa miaka mingi ya kumwasi Mungu imewathibitisha kuwa hawafai lo lote, wala hawawezi kufaa kuingia mbinguni. Utakatifu wa mbinguni na amani yake vingaliwawia mateso makuu. Utukufu wa Mungu, wao ungekuwa moto uteketezao. Wangalitamani kukimbia kutoka mahali hapo patakatifu, hata kutamani kufa kuliko kukaa mbele za yule aliyewafia ili kuwaokoa. Maangamizi ya waovu wanasababishwa na uchaguzi wao wenyewe. Kufungiwa wasikanyage mbinguni kunatokana na hiari yao wenyewe. Mungu ni wa haki na mwenye fadhili. Moto wa siku ya mwisho, sawa na maji ya gharika ya siku za Nuhu, ni hukumu ya Mungu kwa ajili ya maovu ambayo watu walijichagulia kupata. Nia zao zimejizoeza kuasi. Na wanapokufa, hufa na hali ile ile ambayo haibadiliki kuwa na utii. Huwa wenye chuki wala sio upendo.TU 265.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents