Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ufufuo wa Kwanza

  Wale “wanaohesabiwa kuwa wanastahili kuupata ule ufufuo wa wafu” “ni heri na watakatifu” juu yao mauti ya pili haina nguvu. Luka 20:35; Ufunuo 20:6. Lakini wale ambao hawakutubu na kupata msamaha kwa imani, lazima wapokee “msamaha wa dhambi” “adhabu kwa kadiri ya matendo yao” nao watamalizikia katika “mauti ya pili”TU 265.4

  Kwa kuwa haikuwezekana Mungu kumwokoa mdhambi, kwa kuwa hakutaka kuokolewa, basi humwondolea hali ya kutokuishi ambayo uasi wake mwenyewe umeisababisha, na kwa vile amejithibitisha mwenyewe kuwa hafai lolote. “Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo” “Nao watakuwa kama kwamba hawakuwepo kwemwe” Zaburi 37:10; Obadia 16. Watazama huko kusikokuwa na matumaini na kusahauliwa milele.TU 265.5

  Hivyo ndivyo dhambi itakavyokomeshwa. “Umemwangamiza mdhalimu, umelifuta jina lao milele na milele. Adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele” Zab. 9:5-6. Yohana mwandishi wa ufunuo, alisikia nyimbo za sifa zikiimbwa bila machafuko yoyote. Hakuna mpotevu yeyote aliyekuwa akiteswa na kumkufuru Mungu. Hakuna vilio vya mateso vilivyokuwa vikichanganyikana na nyimbo za furaha za kumtukuza Mungu za waliookolewa.TU 266.1

  Juu ya kosa la asili la hali ya umilele, sasa kunakuwa na ufahamu wa kifo. Kama ilivyodhaniwa kuwa kuna mateso ya milele ambayo ni kinyume cha maandiko na mawazo ya binadamu. Kufuata imani ya wengi ni kwamba waliookolewa ambao wako mbinguni wanafahamu mambo yote ya hapa duniani. Lakini itawezekanaje kuwa na furaha kwa wafu kufahamu maisha ya kusumbuka na dhiki waliyo navyo wenyeji wa duniani? Kungekuwa na machukizo sana kujua mtu afapo huingia motoni huko ahera.TU 266.2

  Lakini Biblia inasemaje? Mtu hafahamu neno lo lote wakati afapo. “Pumzi yake hutoka, hurudia udongo wake, siku hiyo mawazo yake hupotea”. “Walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote …. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao hupotea yote pamoja. Wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua. Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kuadhimisha.TU 266.3

  Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako. Aliye hai naam aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo” “Maana mautini hakuna kumbukumu yako, katika kuzimu ni nani atakayekusifu?” Zab. 146:4; Mhubiri 9:5-6; Isaya 38:18-19; Zab. 6:5.TU 266.4

  Siku ya Pentekoste Petro alisema kuwa Daudi “alikufa, akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo” “Maana hututhibitishia kuwa wenye haki wanapokufa hawaendi mbinguni.”TU 266.5

  Paulo alisema “Maana kama watu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. Na kama Kristo hakufufuka imani yenu ni bure: na hao waliolala katika Kristo wamepotea” 1Kor. 15:16-18. Kama kwa muda wa miaka 4000 wenye haki waliokufa wamekwenda mbinguni moja kwa moja, Paulo aliwezaje kusema kuwa, kama hakuna ufufuo, waliolala katika Kristo wamepotea?TU 266.6

  Yesu alipokuwa karibu kuwaacha wanafunzi wake hakuwaambia kuwa watakwenda kwake karibuni, bali alisema, “nakwenda kuwaandalia mahali, nikienda kuwaandalia mahali nitakuja tena, niwakaribisheni kwangu” Yoh. 14:2-3. Paulo anatuambia zaidi kuwa, “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu, nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”. Na kisha aongeza kusema “Basi farijianeni kwa maneno haya” 1 Thes. 4:16-18. Wakati wa kuja kwa Kristo makaburi yatafunguliwa, na waliokufa katika Kristo watafufuliwa ili wapate uzima wa milele.TU 267.1

  Wote watahukumiwa kufuatana na mambo yaliyokuwa yameandikwa vitabuni, nao watapokea thawabu kadiri ya kazi yao ilivyo. Hukumu hii haitendeki wakati mtu afapo. “Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki”. “Angalia, Bwana anakuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, ili afanye hukumu juu ya wale wote”. Matendo 17:31. Yuda 15.TU 267.2

  Sasa, kama watakatifu wako mbinguni tayari, au waovu wamo motoni tayari, kuna maana gani ya kukaa na kuwahukumu watu tena? Maneno ya Mungu yanaweza kufahamiwa na watu wa kawaida. Lakini watu wanyofu hawewezi kuona hekima au haki katika maneno ya kawaida? Je, watu hawa watapewa heko na Bwana, wakiambiwa “Vema mtumishi mwema na mwaminifu, na kuingizwa katika furaha ya Bwana, wakati wameishi muda huo wote? Je, waovu nao watatolewa katika moto, halafu waambiwe ‘Ondokeni kwangu ninyi nyote mtendao maovu?’” Mathayo 25:21,41.TU 267.3

  Mafundisho yale yanayohusu kutokufa kwa roho ni madanganyo yaliyokazwa na kanisa la Rumi, kutokana na imani ya wakafiri. Mafundisho, kutokana na imani ya wakafiri. Mafundisho hayo Luther huyaita hadithi chafu za kipumbavu na udanganyifu mbaya mno, ambazo kanisa la Rumi huzishikilia kama chombo chao cha kupoteza na kupumbaza watu. Biblia hufundisha kuwa watu waliokufa wanalala makaburini mpaka siku ya ufufuo.TU 267.4

  Wenye haki hupumzika katika taabu zao. Kwa muda wa kupumzika ni mfupi tu, ingawa huonekana mrefu. Kwao muda ni mfupi. Wao wanalala, wataamshwa na parapanda ya Mungu ili wapokee hali ya kutokufa. “Maana parapanda Italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu ….. Basi mwili huu wa kuharibika utakapova kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakuwa neno lililoandikwa: mauti imemezwa kwa kushinda” 1Kor. 15:52-54.TU 267.5

  Wakiamshwa kutoka usingizini wa mauti, hawataanza kufikiri mahali walikofia na maisha yao ya mwisho, kabla ya kuingia kaburini. Watakapoamshwa kutoka makaburini kitu cha kwanza watakachoona ni ushindi na kelele za ushindi. “Ku wapi Ewe mauti kushinda kwako? U wapi ewe Mauti ushindi wako? U wapi ewe mauti uchungu wako? Ku wapi Ewe kaburi kushinda kwako?” 1 Kor. 15:55.TU 268.1

  Marejeo: TU 268.2

  E. Peteavel. The Problem of Immorality p. 225.TU 268.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents