Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  34/Mizimu ni Nani Katika Imani ya Roho

  Mafundisho yahusuyo kutokufa kwa roho kwanza yalitokana na imani ya wapagani, na wakati wa giza la kiroho mafundisho haya yaliingizwa katika imani ya kikristo na kuhesabika kuwa ni mojapo ya ukweli, na yakashika mahali pa Maandiko yasemayo kuwa, “wafu hawajui neno lo lote” Mhubiri 9:5. “Watu wengi huamini kuwa roho za wafu ndizo zile, zisemwazo kuwahudumu wale watakaourithi wokovu” Waebrania 1:14.TU 269.1

  Imani ya kuwako roho za wafu kuja kuwahudumia watu wanaoishi, imeandaa njia ya kuingizia mambo ya kisasa ya kuongea na wafu. Kama watu wanaoufahamu unaozidi ule waliokuwa nao wakati walipoishi, mbona hawaji tu kiwazi na kuwaelimisha watu? Ikiwa roho za wafu huwazungukia jamaa zao walioko duniani, mbona hawakai na kuongea nao? Mbona wanaoamini kuwa mtu akifa huwa anajua mambo, hukataa nuru ya Mungu inayoeleza mambo ya roho? Hapa ndipo Shetani hufanyia kazi yake. Malaika waovu huonekana kama wajumbe katika ulimwengu wa roho.TU 269.2

  Mkuu wa uovu yaani shetani anao uwezo wa kuleta sura za watu waliokufa ambao ni jamaa. Maigizo ya watu hao ni kamili kabisa. Huonekana kama wao halisi. Watu wengi hufarijika kuwa ndugu na rafiki zao wako wanaishi huko mbinguni. Bila kujihadhari na hatari yo yote, hutega masikio kwa “roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani” 1 Tim. 4:1.TU 269.3

  Waliokufa bila kujitayarisha, yaani bila kujitoa kwa Kristo, hudai kuwa wako katika furaha kuu huko mbinguni. Watu hawa bandia wanaojidai kuwa wanakaa rahani mbingu, mara nyingine husema maneno ambayo huwa ya kweli. Wakishakuaminiwa, hutoa mafundisho yaliyo kinyume cha Biblia. Kwa kuwa mara nyingine husema maneno ya kweli na kutabiri mambo fulani ambayo hutokea kuwa kweli, hivyo mafundisho yao ya uongo hukubaliwa kama mafundisho ya kweli ya Biblia. Sheria ya Mungu imewekwa kando, na Roho wa neema amedharauliwa. Hiyo ndiyo mizimu, na roho za mashetani. Roho hizi hukataa Uungu wa Kristo na kumhesabu Mwumbaji kuwa na hali sawa na yao.TU 269.4

  Wakati matokeo ya udanganyifu huo hukubaliwa kama ukweli, hutokea ishara ambazo ni kazi za yule mwovu huwadangaya watu wakaziamini kama ishara za Mungu. Watu wengi huamini kuwa hali ya kuongea na wafu. Au mizimu ni ujinga wa kibinadamu. Wanapokabiliwa na maonyesho ya wazi ambayo hawawezi kuyakanusha, hukubali kuwa hayo kutoka kwa Mungu.TU 270.1

  Kwa msaada wa shetani wachawi wa Farao waliigiza kazi ya Mungu na kufanya miujiza. Soma Kutoka 7:10-12. Paulo ashuhudia kuwa kuja kwa Bwana kutatanguliwa na “Kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na maajabu za uongo, na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea” 2Tes. 2:9-10. Yohana naye anasema, “Naye, afanye ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya” ufunuo 13:13-14. Hapa sio ujanja wa kibinadamu unaoelezwa. Watu hudangaywa na shetani kwa ishara ambazo wajumbe wake huzifanya, sio wanazojifanya kuzifanya.TU 270.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents