Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Biblia Huhesabiwa Kama Hadithi

  Mitume, ambao wanaigizwa na roho hizi au mizimu hufanywa watofautiane katika usemi na vile walivyoandika walipokuwa wakiishi duniani. Hivyo ndivyo mizimu huwafanyia wale wanaojifanya kuwa wanaongea na wafu. Shetani huwafanya walimwengu waamini kuwa Biblia ni hadithi tu za kupiga chuku sawa na zinginezo, kinawafaa watoto wa jamii lakini sasa hakifai kutumika siku hizi. Kitabu ambacho kitamhukumu pamoja na wafuasi wake, hukiweka katika kivuli. Mwokozi wa ulimwengu hufananishwa na mtu tu. Wale wanaoamini katika kuongea na roho hizi, hawaoni mwujiza wowote katika maisha ya Mwokozi. Wanasema kuwa miujiza yao inazidi ile ya Kristo alipokuwa hapa duniani.TU 272.2

  Uzungumzaji wa wafu sasa umehesabiwa kuwa dini ya Kikristo, na umevaa sura ya Kikristo, na mafundisho yake hukubaliwa waziwazi. Katika hali yake ya sasa ni ya hatari sana, ya kijanja sana, na ya hila sana. Wenye kuamini hali hiyo hukubali mambo ya Kristo na Biblia, lakini kwa ujanja na hila kubwa. Biblia hutafsiriwa kwa namna ya kupotosha ili iwafurahishe wale wasioongoka. Upendo husisitizwa kuwa ndiyo tabia kuu ya Mungu, lakini hupotoshwa na kumwelekeza katika njia za uasherati. Chuki ya Mungu kuhusu dhambi, na kanuni ya Mungu kuhusu utakatifu hufichwa bila kutajwa. Hadithi huwafanya watu wasione kuwa Biblia ndiyo msingi wa imani yao. Kumkiri Kristo kwa kinywa tu, lakini kwa kweli humkataa kimatendo.TU 272.3

  Ni watu wachache sana ambao wamegundua hila hiyo ya kuongea na mizimu, au wafu. Wengi hujaribu ili kufanya utafiti. Huwa na hali ya hofu juu ya kuongea na roho hizo, lakini huthubutu kwenda mahali palipokatazwa. Hivyo mwovu huwakamata kwa hila na kuwashikilia katika hali ya mateka. Hakuna kinachoweza kuwatoa katika hali hiyo ila maombi ya kweli kweli.TU 272.4

  Watu wanaopendelea kufaya dhambi, hali wanajua kuwa ni dhambi, hujiweka wenyewe katika mikono ya shetani. Hujitenga na Mungu kwa hiari yao, na malaika walizi huwaacha peke yao bila ulinzi.TU 272.5

  “Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunog'ona; je, waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Na waende kwa sheria ya ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi” Isaya 8:19-20.TU 273.1

  Kama watu wamepata mafundisho ya kweli kuhusu hali ya wafu na asili ya mtu, wataona wazi kuwa wenye pepo wanaojidai kuwa waongea na wafu, ni uwezo wa shetani ufanyao kazi ndani yao, kwa maajabu na ishara za uwongo. Lakini watu wengi hufumba macho yao wasione nuru kuhusu jambo hili, na shetani huwafunikiza nawavu wake. “Kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu amewaleta nguvu ya upotevu, wauamini uwongo” 2 Thes. 2:10-11.TU 273.2

  Wale wanaopinga mambo ya pepo humshambulia Shetani na mamlaka zake. Shetani hatakubali kushindwa hata kidogo, isipokuwa afukuzwe na wajumbe wa mbinguni. Atataja Maandiko hali akiyapotosha, ili ashinde. Watu watakaoshinda hatari ya wakati huu, lazima wafahamu ushuhuda wa Maandiko barabara.TU 273.3

  Roho za mashetani, hujionyesha kama ndugu na marafiki wa watu ambao walikufa, hutujia na kutushauri mambo fulani fulani. Halafu hufanya maajabu. Lazima tuwapinge kwa Biblia na ukweli wake, kwamba wafu hawajui neno lolote, kwa hiyo hawa wanaaonekana kama kwamba ni jamaa zetu waliokufa ni roho za mashetani yaani pepo.TU 273.4

  Wale ambao imani yao haikujengeka kwa neno la Mungu, yaani Biblia, watadanganyika na kupotezwa na shetani. Maana Shetani hufanya kazi yake kwa madanganyo yote ya upotevu, na madangayo haya yatazidi kadiri tunavyokaribia mwisho. Lakini wote wanaotafuta ukweli wa Biblia na kutakasa roho zao kwa njia ya kulitii neno la Mungu, watashinda. Mwokozi atawatumia malaika wote wa mbinguni kuwalinda. Hatamwaacha hata mtu wake mmoja ashindwe na Shetani. Wale wanaojifariji kwamba hakuna adhabu yo yote itakayowapata wenye dhambi, na kudharau maonyo ya mbinguni watapotezwa na udanganyifu wa shetani katika mizimu na kuangamia.TU 273.5

  Wenye mizaha wataendelea kukataa maonyo ya mbinguni, kuhusu mpango wa wokovu na adhabu itakayowapata katika mizimu wanaoikataa kweli, na kujiona wako salama. Watatajihafifisha kabisa, kiasi cha kutojali sheria ya Mungu. Kadiri walivyojiunga na shetani, itakuwa vigumu kujitenga naye na hila zake.TU 273.6

  Msingi wa kazi ya shetani ni ule uliowekwa katika Edeni kwa Hawa, kwamba, “Kufa hamtakufa” “Siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafumbuliwa, na mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya” Mwanzo. 3:4-5. Madangayifu yake yatafikia mpaka kwenye masalio ya mwisho ya Mungu. Nabii asema, “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura …. Hizo ndizo roho za mashetani zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote, kuwakusanya kwa vita vya siku ile kuu ya Mungu Mwenyenzi.”TU 274.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents