Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  35/ Uhuru wa Dhamiri Unatishwa

  Sasa makanisa ya Kiprotestanti yanaliona kanisa la Kirumi kuwa rafiki yao zaidi ya walivyoliona katika miaka iliyopita. Katia nchi hizo, ambako ukatoliki umeenea sana, mawazo ya wengi huona kuwa tofauti kati yetu na wao sio kubwa, bali katika mambo makuu ya imani tunakubalina nao, ila kuwa vipengele vidogo tu vikirekebishwa, tutakubalina nao katika mambo yote. Kulikuwako nyakati hapo zamani, Waprotestanti walipowafundisha watoto wao kuwa kukubaliana na wakatoliki kidini kumwasi Mungu. Sasa hali ya maoni yao inatofauti kiasi gani!TU 275.1

  Watetezi wa Ukatoliki husema kuwa kanisa lilifanya vibaya sana kufikiri kuwa waprotestanti walikuwa wapotofu. Hizi zilikuwa zama za giza, za ujinga. Wanalaumu ukatili waliowatendea watu kuwa ulikuwa wa kinyama wakati huo.TU 275.2

  Je, watu hawa sasa wamesahau madai yao kuwa wao (Kansia la Rumi) hawakosi? Kanisa la Kirumi hudai kwamba, “kanisa halikosi kamwe, wala halitakosa kamwe. Hivyo ndivyo Maanandiko yanavyosema.”TU 275.3

  Kanisa la mapapa halitapunguza madai yake kuwa halikosi. Ngoja serikali izuie mambo ya ukatili sana, baadaye Rumi ikapata uwezo wake wa kwanza itafufua hali yake ya mateso.TU 275.4

  Ni kweli kwamba wako wakristo halisi katika kanisa la Rumi. Watu maelfu wanamtumikia Mungu kwa kadiri ya ujuzi walio nao katika kanisa hilo. Mungu huwaangalia kwa huruma watu hao. Wao wamepotoshwa na kufundishwa kinyume cha ukweli. Mungu atawaletea nuru, na wengi watajiunga pamoja na watu wake, katika kanisa la kweli.TU 275.5

  Lakini kama kanuni za Ukatoliki zilivyo, wanaachana na Biblia kabisa, sawa kama walivyokuwa hapo kwanza.TU 275.6

  Kanisa la Rumi hutumia kila njia ili lipate kukubalika katika ulimwengu, ili liweze kurudisha hali yake ya zamani ya kutesa, na kuvuruga mambo yote ya Kiprotestant.TU 275.7

  Wakatoliki wanaendelea kufaulu katika makusudi yao. Angalia jinsi makanisa yao yanavyozidi kuongezeka na tazama Koleji zao na vyuo vyao vinavyozidi na kujazwa na wanafunzi wa Kiprotestanti. Angalia jinsi kawaida zao za ibada zinavyoongezeka huko Uingereza, na maasi yanavyozidi kwa upande wa wakuu wa Katoliki.TU 275.8

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents