Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utunzaji wa Jumapili

  Utunzaji wa Jumapili ni desturi iliyoanzishwa na kanisa la Rumi, ambayo hujidai kuwa hiyo ndiyo alama ya uwezo wake. Roho ya Upapa, ambayo ni ya kujiambatanisha na ulimwengu, na desturi zake za kujali mapokeo ya wanadamu zaidi ya sheria za Mungu, roho hiyo hiyo imeenea katika makanisa ya Kiprotestanti na kuwaongoza kushika Jumapili kama Warumi walivyofanya zamani.TU 279.5

  Amri za kitawala na za mabaraza, pamoja na mpango ya kanisa na kanuni zake, ambazo zilisaidiwa na serikali ndizo zilikuwa hatua za kuingiza ukafiri katika makanisa ya Kiristo, na kuheshimiwa na ulimwengu. Hatua ya kwanza ya kuiheshimu Jumapili, ilikuwa amri iliyotolewa na mfalme Constantine. Ingawa ilikuwa karibu kuwa kawaida ya kishenzi, ilisisitizwa na mfalme iwekwe katika upande wa dini, baada ya kuongokaTU 280.1

  Eusebius, kasisi aliyetafuta msaada wa serikali ili atekeleze mambo ya kanisa, na ambaye alikuwa rafiki mpendwa wa mfalme Constantine, ndiye alieneza habari kuwa Kristo amehamisha heshima ya Sabato kutoka Jumamosi na kuiweka Jumapili. Hakuwa na ushahidi wa Biblia kuhusu madai hayo. Eusebius mwenyewe alikiri kuwa ni uongo bila kujua kuwa anakiri. Alisema, “Mambo yote yaliyopaswa kutendeka siku ya Sabato yalihamishiwa katika siku ya Jumapili, yaani siku ya Bwana”.TU 280.2

  Upapa ulipoimarika, utunzaji wa Jumapili uliendelea. Kwa muda, siku ya saba iliendelea kuheshimiwa kama Sabato, lakini badiliko lilikuwa linafanyika. Baadaye papa aliamuru kwamba wakuu wa majimbo, lazima wawaadhibu wote wanaovunja Jumapili wasije wakaleta balaa kwao wenyewe na majirani.TU 280.3

  Maagizo ya mabaraza ya kanisa, hayakutosha, hivyo walitafuta msaada wa serikali ili amri ya kutofanya kazi Jumapili ikazwe kisheria. Katika baraza la wakuu lililofanyika Rumi, lilirudia mashauri yote yahusuyo kutunza Jumapili, yaliyofanyika nyuma, na kuyakaza upya, kuwa amri ya kanisa likikazwa na mamlaka ya serikali.TU 280.4

  Hata hivyo kutokuwako na fungu la Biblia linalounga mkono juu ya utunzaji wa Jumapili, kulizidi kuwatia wasiwasi. Watu waliuliza sababu ya kupuuza usemi wa Mungu, unaoamuru, “Lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako” na kuheshimu siku ya jua. Kwa kuwa walikosa fungu la Biblia la kuthibitisha, walitoa maelezo yo yote waliyoona kuwa yanafaa.TU 280.5

  Mtu mwenye juhudi ya kusisitiza utunzaji wa Jumapili, alitembelea Uingereza mwishoni mwa karne ya kumi na mbili mtu huyo alipofika katika makanisa ya huko na kufundisha mambo hayo, alipingwa vibaya na mashahidi waaminifu wa ukweli, na kwa kuwa hakupata matunda, aliondoka kwa muda. Baadaye aliporudi tena alikuja na maandiko aliyodai kuwa yametoka kwa Mungu mwenyewe. Maandiko hayo yalikuwa yanasema juu ya utunzaji wa Jumapili, na kwamba mtu yeyote atakayepinga utunzaji huo ataona cha mtema kuni, maandiko haya ilisememekana kuwa yameanguka kutoka mbinguni, kwamba yalikutwa juu ya madhabahu ya kanisla la Simeon huko Yerusalemu, kwenye kilima cha Golgota. Lakini kwa kweli yaliandikwa na papa wa Rumi. Hila zote za udanganyifu vimekuwa vikifanywa na mapapa wa Rumi.TU 280.6

  Lakini juhudi zote za kuimarisha utunzaji wa Jumapili kuwa sabato zimetokana na mapapa ambao hukiri wazi sabato iliwekwa na Mungu. Katika karne ya kumi na sita, baraza la mapapa lilitangaza hivi: “Wakristo wote wajue kuwa siku ya saba ya juma ilitoka kwa na Mungu mwenyewe, nayo imekuwa ikitunzwa siku zote, wala si Wayahudi peke yao, bali na watu wote wanaokiri kumwabudu Mungu; ingawa sisi wakristo tumeibadili Sabato na kuifanya iwe jumapili, ambayo ndiyo siku ya Bwana” Wale walioharibu amri ya Mungu, walijua aina ya kazi yao.TU 281.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents