Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mnyama Mwenye Pembe Mbili Kama Kondoo

  Unabii wa Ufunuo 13 unasema kuwa mnyama afananaye na mwana kondoo mwenye pembe mbili, utawafanya watu wote wakaao duniani wamsujudie papa ambaye afananishwa na mnyama kama chui. Mnyama afananaye na mwanakondoo atawaambia watu wakaao duniani wamfanyie mnyama chui sanamu. Zaidi ya hayo mnyama huyu atawaamuru watu, wadogo na wakubwa matajiri na maskini, walio huru na wafungwa, wadogo na wakubwa, matajiri maskini, walio huru na wafungwa watiwe alama ya mnyama. Ufunuo 13:11-16. Marekani ndiyo inayofananishwa na mnyama kama mwanakondoo, mwenye pembe mbili. Unabii huu utatimia wakati Marekani itakapolazimisha watu washike Jumapili ambayo Rumi hudai kuwa ndiyo alama ya ukuu wake. “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule” ufunuo 13:3. Pigo la mauti linaelekeza kwenye anguko la upapa la mwaka 1798. Baada ya haya, unabii husema, “pigo lake la mauti lilipona, dunia yote ikamstaajabia mnyama yule”. Paulo asema kuwa “mtu wa dhambi” atatenda kazi yake ya udanganyifu mpaka mwisho wa wakati 2 Thes. 2:3-8. “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudia, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana kondoo”. Ufunuo 13:8. Katika nchi zote za dunia papa atatukuzwa kwa ajili ya Jumapili aliyoibuni.TU 282.1

  Tangu kati ya karne ya kumi na tisa wanafunzi wa Biblia walileta ushuhuda huu ulimwenguni. Sasa utimizo wa unabii huu unaonekana kuwa unaharakisha sana kutimizwa kwake. Hata walimu wa Kiprotestanti wanakutimizwa kwake. Hata walimu wa Kiprotestanti wanakubaliana na mamlaka hii iliyoweka Jumapili kuwa sabato, na wala hawana fungu la Biblia linalowaunga mkono, sawa kama wakatoliki walivyokosa fungu. Thibitisho kuwa hukumu ya Mungu itawaangukia washikao Jumapili, litarudiwa tena na hata sasa hukumu ya Mungu inaanza kuharakisha.TU 282.2

  Kanisa la Rumi lina werevu sana. Linasoma mambo yanayoonekana kuwa kwamba makanisa ya Kiprotestanti yanaliheshimu, kwa vile yanakubali kushika jumapili, ambayo ni sabato ya uongo, na kwamba linajitayarisha kulazimisha watu kuishika Jumapili kwa nguvu, kwa kutumia njia zile zile zilizotumika zamani. Jinsi litakavyokuwa tayari kuunga mkono Uprotestanti ili kutimizia shabaha yake ni wazi.TU 282.3

  Kanisa la katoliki limebuni shirika kuu linalosimamiwa na papa. Washiriki au ajumbe wake, ambao ni mamilioni wako kila nchi, na kila mahali, wote wakiwasiliana na papa, bila kujali taifa gani au serikali gani wao waliomo. Ingawa hula kiapo cha kutumikia nchi na serikali yao lakini kwa chini chini huwa na kiapo kingine cha kutimiza maazimio ya papa wa Rumi.TU 283.1

  Historia inaonyesha jinsi kanisa hili linavyojihusisha na mambo mbalimbali ya nchi na mataifa mbalimbali. Hivyo hufaulu kuingilia mambo hata ya mapinduzi ya watawala, ili mradi watimize makusudi yao.TU 283.2

  Wanajivuna kuwa wao hawabadiliki kwa vyo vyote. Waprotestanti wanajua kidogo sana kuhusu mhimizo wao wa mwungano wa dini, kwamba Rumi ina makusudi mbalimbali vile hawa wanavyodhani. Hata kule kushika Jumapili hawana habari juu yake.TU 283.3

  Waprotestanti wanaposhughulika na kutafuta mwungano wa Rumi, Warumi wao hushughulika na jinsi ya kujiimarisha na kushika uwezo wote mikononi mwao, ule waliokuwa nao zamani, ambao uliwapotea. Kusudi lao ni kuweza kuwa na uwezo wa kutawala kanisa na serikali pia, ili ikiwezekana kwamba matakwa ya kanisa yaweze kutimizwa kwa nguvu ya serikali, si muda mrefu ujao mwungano baina ya kanisa na serikali utafikiwa, na hapo ushindi wa Rumi utakamilika. Mwungano wa makanisa ya Kiprotestanti kwanza; halafu mwungano wa makanisa ya Kiprotestanti na Rumi; mwisho, mwungano wa kanisa na serikali.TU 283.4

  Makanisa ya Kiprotestanit yatakuja kung'amua makusudi ya Rumi, yakiwa yamechelewa tayari, wala hayataweza kujitoa mtegoni. Kanisa la Rumi linaendelea kupata uwezo kimya kimya. Mvuto wao unaingia katika majumba ya kutunga sheria, makanisa, na katika mioyo ya watu. Wanajiimarisha ili waweze kukamilisha maazimio yao; wakati ukifika watatenda mambo yao. Mambo yao ni kupigana vita na Mungu na neno lake. Hivi kila mwenye kutii neno la Mungu atakabiliana na mashutumu na mateso.TU 283.5

  Marejeo: TU 283.6

  John L. Von Mosheim — Institutes of Eccelesistical History Book 3 Century II, sehemu ya 2 sura kifungu 9 Note 17. TU 283.7

  Robert Cox Sabbath laws and Sabbath Duties p. 558 TU 283.8

  Angalia Heylyn. History of the Sabbath pt. 2 sura 5 sec 7. TU 283.9

  Thomas Morer — Discourse in Six Dialogues on the Name, nation and Observation of the Lord’s Day pp. 281, 282 TU 283.10

  Angalia Michael Geddes Church History of Ethiopia pp. 311, 312. TU 283.11

  Angalia kwa ajili ya mfano John Dowling. The History of Romaism bk. 5, sura 6 sec 55 and Mosheim bk 3 cent 11 part 2 chap. 2 see sec. 9 note 17.TU 283.12

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents