Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ulevi umewafumba Wengi

  Mahakama yamechafuka na kuwa mahali pa ufedhuli, watawala wamekumbwa na tamaa ya kupata faida ya haramu pamoja na uasherati. Ulevi wa pombe na kutokuwa na kiasi vimewafumba watu wengi wasitambue lo lote, kwa hiyo shetani amewatawala kabisa. Mahakimu wanaongoza katika kula rushwa. Ulevi wa kila aina, utovu wa uaminifu, vimewatawala wanasheria. Na sasa kwa vile shetani hawezi kuwashikilia walimwengu ili waache kusoma Maandiko matakatifu amebuni njia nyingine ili apate kukamilisha kazi yake. Kuharibu imani za watu wasiamini Biblia pia sawa na kuiharibu Biblia yenyewe.TU 285.4

  Kama ilivyokuwa hapo mwanzoni, amefanya kazi yake ya upotovu kupitia katika makanisa. Katika kupotosha Maandiko, amewaongoza kutafsiri vibaya mafungu ya Biblia, na kwa hali hiyo amepanda mbegu za ukafiri kwa watu. Watu wakishikilia maneno ya Wakatoliki kuwa mtu afapo, roho yake haifi, wamekataa maneno ya kweli ya msingi ambao Mungu ameuweka, wakaandamana na mapotofu ya giza, kwa hiyo hawezi kuepushwa na udanganyifu wa pepo wanaojifanya kuwa ni jamaa za watu waliokufa wanaowatembelea walio hai. Mafundisho ya kwamba kuna moto wa milele unaowaunguza watu wakati wanapokufa, yamewapotosha wengi wauache ukweli wa Biblia. Kama amri ya nne inavyohimiza, inaonekana kuwa utunzaji wa Sabato ya siku ya saba unalazimishwa, na kwa kuwa hawapendi kufanya hivyo, walimu wanaopendwa na watu wake wameitupilia mbali sheria ya Mungu pamoja na sabato. Kwa kadiri msistizo wa sabato unavyoenea, kuikataa sabato pia kutaenea ulimwenguni. Viongozi wa makanisa wanafungua milango ili ukafiri uingie, na kuamini pepo na kukataa sheria ya Mungu. Kuna hali ya kutisha ya umizimu katika makanisa ya kikristo leo, katika ulimwengu.TU 286.1

  Hata hivyo, watu hawa wanajidai kuwa kule kushika Jumapili kutaleta uheri katika jamii. Ni kusudi la shetani kuchanganya kweli na uongo, halafu kuwafanya watu wajione kuwa wanaridhika na hali hiyo. Wanaosisitiza ushikaji wa Jumapili wanaweza kutangaza matengenezo watu wanayotaka wakiunganisha ukweli wa Biblia, ambao huwa kinyume cha sheria ya Mungu. Watumishi wa Mungu hawawezi kujiunga na watu wa jinsi hii. Hakuna kitu kinachotosheleza kutoa sheria ya Mungu na kuweka kitu kingine, ambacho ni cha mwanadamu.TU 286.2

  Shetani atawaingiza watu katika madangayo yake kwa njia ya makosa mawili makuu, yaani kosa la kwanza ni lile la kutokufa kwa roho, na kosa la pili ni kushika jumapili badala ya sabato ya siku ya saba. Shetani ataweka watu katika udanganyifu wake. Kosa la kwanza huweka msingi wa kuongea na wafu, na kosa la pili hutia kifungo cha kuwafungamanisha na Rumi. Waprotestanti wa Marekani watakuwa wa kwanza kunyosha mikono yao kuvusha ghuba na kuunganisha na uongeaji wa wafu; wataunganika na Rumi; na chini ya nguvu hizi tatu, nchi hii itafuata nyayo za Rumi za kutawala uhuru wa dhamiri. Kwa vile imani ya kuongea na wafu, itajifananisha na dini ya kikristo ya kisasa, itakuwa na uwezo wa kudanganya. Shetani mwenyewe atajigeuza kuwa mfano wa malaika wa nuru. Kwa njia ya pepo hao wa kuongea, miujiza itafanyika, wagonjwa watapona, na ishara nyingi zisizoweza kukanushwa zitatendeka.TU 286.3

  Mapapa ambao hujidai kuwa dini ya kweli hujulikana kwa ishara hizo watadanganyika kabisa kwa ishara hizo, na Waprotestanti wakiwa wametupa ngao ya ukweli, wao pia watadanganywa. Wakatoliki, Waprotestanti na walimwengu wote wataona katika mwungano huo kuwa ulimwengu unaongolewa na Kristo.TU 287.1

  Kwa njia ya pepo hawa Shetani ataonekana kana kwamba ndiye mfadhili wa wanadamu, akiwaponya wagonjwa na kuwaletea dini ya namna mpya, lakini wakati ule ule akiwapeleka watu katika uharibifu. Ulevi huaribu uwezo wa kufikiri. Kupenda anasa na uasherati, ugomvi na kumwaga damu ndiyo matokeo yake.TU 287.2

  Vita husisimua tamaa mbaya ya rohoni na kuingiza hali hiyo mpaka ndani, kwenye damu. Ni kusudi la shetani kuwachochea mataifa wapigane, ili kuwazuia wasijiandae kusimama mbele za Mungu.TU 287.3

  Shetani amejifunza siri za vitu vya asili, naye anaweza kutumia vitu vya asili ili kuleta madhara kwa kadiri ile Mungu aruhusuvyo. Mungu ndiye huzuia madhara yanayoweza kuletwa na shetani kwa viumbe vyake. Lakini wakristo wameidharau sheria yake, naye atafanya kama alivyosema, yaani ataondoa ulinzi wake kwao na kuwaacha watupu bila kinga. Shetani huwashika wale ambao Mungu amewaondolea ulinzi wake. Atawafanikisha wengine na wengine kuwapa taabu ili wapate kumlaumu Mungu, kuwa ndiye anasababisha taabu yao. Hayo yote huyatenda ili kuendeleza kazi yake ya udanganyifu.TU 287.4

  Wakati shetani anapojidai kuwa ni mfadhili wa watu wakati ule ule huwaletea magonjwa na dhiki kubwa mpaka wengi waangamie, na miji mikubwa ibaki katika maganjo matupu. Ajali zinazotokea katika bahari na nchi kavu.TU 287.5

  Katika milipuko ya moto, katika tufani na dhoruba katika matetemeko ya nchi, na katika kuumuka kwa mawimbi, na mafuriko makubwa na mambo mengi ya kutisha yanayoangamiza maisha ya watu, shetani hutumia uwezo wake ajionyeshe alivyo. Hugharikisha mavuno mashambani, ili kusababisha njaa. Hukoroga hewa na kuwa ya hatari iwezayo kuangamiza watu maelfu.TU 288.1

  Kisa mwovu mkuu huyo huwasingizia watu wanaoshika amri za Mungu kuwa ndio wanaosababisha maafa hayo yote. Pia husema kwamba kwa sababu watu wamemkosea Mungu kwa kutoshika siku ya Jumapili, ndiyo sababu ya kutokea mambo haya, nayo hayatakoma mpaka siku ya jumapili itakapoheshimiwa na kushikwa barabara. Wale wanaoasi siku ya jumapili huzuia mibaraka ya Mungu. Kwa hiyo mashitaka waliyoshitakiwa watu wa Mungu zamani, yatarudiwa tena. “Wakati Ahabu alipomwona Eliya ….. Ahabu alimwambia wewe ndiye unayetaabisha Israeli?” 1Fal. 18:17-18. Uwezo wa kutenda miujiza utawavutia watu kuwaelekeza kwa wale wanaomtii Mungu kuliko jumuia. Roho watamwaambia kuwa wametumwa na Mungu ili kuwahakikishia kuwa, wale wanaopinga utunzaji wa jumapili wanafanya makosa. Watauombolezea uovu uliomo ulimwenguni, na ushuhuda wa pili wa walimu wa dini walivyohafifisha hali ya kiroho kwa kutoiheshimu jumapili.TU 288.2

  Chini ya uongozi wa Rumi, wale walioteseka kwa ajli ya Injili walishutumiwa kama watenda maovu, wakihesabiwa katika jamaa ya Shetani. Hivyo ndivyo itakavyokuwa sasa. Shetani atawaletea mateso wale wanaoshika sheria ya Mungu, ili washitakiwe kuwa ndio wanaosababisha maafa duniani. Atajitahidi kuwatisha kwa njia ya hofu, akiwachochea watu pamoja na serikali wapingane na sheria ya Mungu.TU 288.3

  Wale wanaoiheshimu sabato ya Biblia watashutumiwa kuwa ni maadui wa nchi, na wavunja sheria, ya jamii, Ni watu wakorofi wasio na utaratibu, nao ndio wanaosababisha maafa haya yote. Watashitakiwa kama wahaini, walio kinyume cha serikali. Wachungaji wanaovunja sheria ya Mungu, hujipendekeza kana kwamba ni wapenzi wa serikali. Katika majumba ya kutunga sheria na katika mahakama, watunza amri za Mungu watashutumiwa, Watatajwa vibaya kila mahali na wapakwa matope katika mambo yao yote, kwa uongo.TU 288.4

  Wakuu wa kanisa na waongozi wa serikali watashirikiana kuwalazimisha watu wote kushika Jumapili. Hata watu wa Marekani, ambao ni nchi huru, watu watajitolea kufuata mkumbo wa wengi na kulazimisha watu kushika jumapili. Uhuru wa dhamiri ambao umegharimu gharama kuu, hautaheshimiwa, wala kujaliwa. Wakati wa mapambano yaliyo karibuni, tutaona maneno ya nabii yasemayo, “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu” Ufunuo 12:17.TU 288.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents