Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  37/Usalama Wetu wa Pekee

  Watu wa Mungu wameelekezwa kwa Neno la Mungu kuwa ndilo litakuwa usalama wao katika udanganyifu wa giza. Shetani hutumia kila njia anayobuni ili kuwafanya watu wasipate ukweli wa Biblia. Kila mara kazi ya Mungu inapoanzishwa, yeye naye huamka kwa juhudi ili kuinga. Mapambano ya mwisho baina ya Kristo na wafuasi wake karibu yatatokea waziwazi, mbele yetu. Shetani ataigiza mambo yafanane na yale ya kweli, mpaka itakuwa vigumu kupagundua, isipokuwa kwa njia ya Maandiko matakatifu peke yake.TU 290.1

  Wale wanaojitahidi kushika amri za Mungu, watapingwa na kudhihakiwa. Ili kusudi waweze kusimama na kushinda, ni lazima wafahamu mapenzi ya Mungu jinsi yalivyofunuliwa katika Biblia. Wataweza kumheshimu tu wakiwa na ufahamu wa kweli kuhusu tabia yake serikali yake, na makusudi yake; halafu watende kama yalivyo. Hakuna wengine, isipokuwa wale waliojiimarisha kiroho kwa njia ya ukweli wa Biblia, ndio watafaulu katika mapambano ya mwisho.TU 290.2

  Kabla mwokozi hajasulubishwa aliwaeleza wanafunzi wake kwamba, atauawa na kufufuka tena. Malaika waliokuwako ili kuyakazia maneno yake katika mioyo ya watu. Lakini maneno yake yalitoweka katika mioyo ya wanafunzi wake, na wakati jaribu lilipokuja, na Yesu alipokufa, matumaini yao yalitoweka, wakafanana kama kwamba hawakuonywa juu ya mambo hayo. Vivyo hivyo unabii umetufunulia mambo yajayo waziwazi, kama wanafunzi walivyofunuliwa na Kristo. Mungu anapotuma maonyo, hutazamia kuwa kila mtu atatega sikio na kuyajali, lakini makundi mengi hawaelewi ukweli huu muhimu na wakati wa taabu utawapata bila kuwa tayari. Adhabu ya kutisha itakayowaangukia watakaomwabudu mnyama na sanamu yake (Ufunuo 14:9-11) ingewafanya watu waamke na kuchunguza maana ya alama ya mnyama, na jinsi ya kujiepusha nayo. Lakini watu hawashughuliki na ukweli wa Biblia na mafundisho yake, kwa sababu huwapa kile wanachotaka, yaani udanganyifu.TU 290.3

  Lakini Mungu atakuwa na watu wenye kushika Biblia na mafundisho yake peke yake, kuwa ndiyo kanuni ya maisha ya msingi wa matengenezo yote. Mawazo ya wataalamu, na tafsiri potofu za Biblia wanazoeleza watu wa sayansi, na mashauri yanayofanywa na kuamuriwa na mabaraza kwa kura ya wengi, hata mojawapo lisingefikiriwa kuwa ushahidi wa mafundisho. Sisi tungeshikilia neno kuwa, “Ndivyo asemavyo Bwana” Shetani anawatazamisha watu kwa wachungaji wao, na wataalamu wa theolojia kuwa ndio wanaotosha kuwaongoza, badala ya kuangalia Biblia na kujisomea wenyewe. Kwa vile anavyowaongoza wawategemee viongozi hawa, basi anawavuta wengi.TU 290.4

  Kristo alipokuja watu wa kawaida tu walimsikiliza kwa furaha. Lakini wakuu wa makuhani waongozi wa watu, walizama katika chuki, wakamkataa masihi. Waliuliza, Inakuwaje watawala wetu na wenye maarifa na akili hawamwamini Yesu? Walimu hao waliongoza taifa la Kiyahudi kumkataa Mkombozi.TU 291.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents