Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wajibu wa Kwanza wa Mkuu

  Kuwa na nia njema peke yake …. Na kufanya kama vile mchungaji anavyomwambi kuwa ndivyo haki hakutoshi.TU 292.3

  Inampasa kila mtu kuchunguza maandiko kwa ajili yake mwenyewe. Humo ataona vibao vinavyooneysha baraka ya mbinguni na wala asibahatishe.TU 292.4

  Ni wajibu, tena wajibu mkuu wa kila mtu kujifunza kutoka katika Maandiko ili apate kujua ukweli wa Mungu ulivyo, halafu atembee katika nuru ya ukweli huo; na kuwa na mawazo yetu wenyewe, kwa vile tutakavyosimama wenyewe mbele za Mungu.TU 292.5

  Watu wasomi pamoja na majivuno yao ya hekima, hufundisha kuwa Maandiko yanazungumza kwa njia ya siri sana, na lugha ya kifumambofumbo isiyoeleweka kwa watu wa kawaida. Watu hawa ni waalimu wa uongo. Lugha ya Biblia ingeelezwa kwa maana yake hasa kama ilivyoandikwa, isipokuwa pale mifano, au vielelezo vilipotumiwa. Kama watu wangeichukua Biblia jinsi ilivyo, kama inavyosomeka, kazi ya kuwaleta watu maelfu zizini mwa Kristo, ingekamilika. Watu hao ambao sasa wanatangatanga katika makosa.TU 292.6

  Maandiko mengi ambayo wataalamu huyapitia bila kuyajali, humfaa sana kumfariji, mtu yule aliyejifunza katika skuli ya Kristo. Kuielewa Biblia hakutegemei akili ya mtu na elimu aliye nayo, bali hutegemea jinsi mtu anavyotia nia yake, na kuwa na kiu ya haki ya Neno la Mungu.TU 292.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents