Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Matokeo ya Kutosoma Biblia na Kuomba.

  Biblia isingalisomwa kamwe bila kuomba. Roho Mtakatifu pekee ndiye hutuwezesha na kutufanya tufahamu mambo ya Biblia, au kutuzuia tusiny'ang'anywe ujumbe unaoonekana kama mgumu. Malaika wa Mungu huandaa mioyo ili kulipokea Neno la Mungu. Tutapendezwa na uzuri wake, na kuimarishwa na ahadi zake. Majaribu kila mara huonekana kana kwamba ni magumu, kwa sababu mwenye kujaribiwa huwa hakumbuki ahadi za Mungu, na kukutana akiwa na silaha ya Maandiko Matakatifu. Lakini malaika wa Mungu huzungukia wale walio tayari kufundishwa, na watawakumbusha ukweli wanaouhitaji. “Atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” Yoha. 14:26. Lakini mafundisho ya Kristo lazima yawe yameota kamili mioyoni, ndipo Roho mtakatifu apate kuwakumbusha, wakati wa hatari.TU 292.8

  Mambo ya mwisho ya dunia iliyojaa watu karibu kuamuliwa. Kila mfuasi wa Kristo lazima aulize, “Bwana unataka nifanye nini?” Matendo 9:6. Lazima sasa tutafute kwa uhakika kuwa na mambo makuu ya Mungu katika maisha yetu. Hatuna muda wa kupoteza. Tumo katika ardhi ya shetani. Msilale enyi walinzi wa Mungu.TU 293.1

  Wengi hujifariji kwamba hawafanyi makosa kadha wa kadha. Kule kuwa mti katika bustani ya Mungu hakutoshi. Lazima wazae matunda. Katika vitabu vya mbinguni watu hawa huandikwa kama wanaoharibu ardhi. Walakini wale ambao wameidharau rehema ya Mungu na kushutumu neema yake upendo na uvumilivu wa Mungu bado unawashughulikia.TU 293.2

  Wakati wa kiangazi miti yote huwa haina tofauti, ya kijani na mingine lakini wakati wa baridi ukifika, miti ya kijani hubaki katika hali ile ile na mingine hupukutisha kabisa majani yake. Hebu upinzani wa aina fulani utokee, hebu dhiki itokee, hebu mateso yachemke, wakati huo wanafiki na wajipendekezao wote watakana imani yao, lakini wakrsito wa kweli watasimama imara, imani yao itadumu kuwa imara, matumaini yao yatang'aa kuliko wakati wa raha na mafanikio.TU 293.3

  “Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao mizizi yake karibu na mto; hautaona hofu wakati wa hari ujapo; basi jani lake litakuwa bichi, wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda”. Yeremia 17:8.TU 293.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents