Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kushambulia Ufalme wa Shetani.

  Wahubiri wa Vaudois waliendelea kutoa sehemu za Maandiko Matakatifu kwa uangalifu. Nuru ya Injili ilipenya kwa watu wengi, mpaka Jua la haki likang'aa mioyoni mwa watu kwa nguvu za kuponya. Kila mara aliyesikia neno alitamani apate sehemu ya Maandiko, ili ahakikishe yale aliyosikia.TU 27.1

  Wengi waliona upuuzi wa maombezi ya watu yaliyofanywa na mapadri kwa wenye dhambi. Wengi walisema kwa furaha, “Kristo ndiye Kuhani wangu. Damu yake ndiyo kafara yangu, madhabahu yake ndilo ungamo langu” Kwa hiyo nuru kuu iliwaangazia watu wengi, ambao ilionekana kana kwamba inawapeleka mbinguni. Hofu yote ya kifo ilitoweka. Sasa walikuwa tayari kuingia gerezani, ikilazimu kwa ajili ya Mwokozi wao.TU 27.2

  Neno la Mungu lilisomwa kwa siri, wakati fulani kwa mtu mmoja tu pengine kwa kikundi cha watu, kilichotamani kupata nuru. Wakati mwingine usiku kucha ulitumika kwa kujifunza Biblia kwa njia hiyo. Mara nyingi maneno haya yalitamkwa: “Je, Mungu ataikubali kafara yangu? Je, ataifurahia? Je, atanisamehe?” Majibu kwa maswali hayo yalisomwa: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” Mathayo 11:28.TU 27.3

  Wahubiri hao walirudi nyumbani kwao kwa furaha ili kuendeleza nuru ya Injili, na kuwasimulia wenzao mambo waliyoona. Waligundua njia safi ya kuwafurahisha na kuwafariji. Maandiko matakatifu yalizungumza katika roho za watu walioyatamini.TU 27.4

  Mjumbe wa kweli alikwenda zake. Na mara nyingi hakuulizwa kama atarudi au hatarudi. Watu walikuwa wamejazwa na furaha ya mshangao hata hawakuwa na nafasi ya kumwuliza maswali. Walijiuliza kwamba: Huenda akawa ni malaika aliyetoka mbinguni?TU 27.5

  Wakati mwingine mjumbe wa Injili atakuwa amekwenda katika nchi nyingine, au anateseka gerezani, au amekwisha kufia dini na mifupa yake imetawanyika. Lakini maneno anayoyasema kabla ya kuondoka yanaendelea kutenda kazi.TU 27.6

  Waongozi wa kipapa waliona hatari itokanayo na watumishi hawa wa Mungu. Waliona kuwa nuru ya Injili inayomulikwa na watu hao itaweza kuenea na kuondoa giza ilililowafunika watu. Nuru hiyo itawaelekeza watu kwa Mungu peke yake, na kuharibu majivuno ya Rumi.TU 27.7

  Watu hawa walioshikilia imani ya kanisa la kwanza walikuwa ushindi wa kufunua uongo wa Rumi na uasi wake. Kwa hiyo chuki na mateso yalitokea. Kule kung'ang'ania ukweli wa biblia kukataa kukubaliana na Rumi, kulichemsha chuki na vita.TU 28.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents