Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Watu wa Mungu hawapotoshwi

  Lakini watu wa Mungu hawatapotoshwa. Mafundisho ya huyu kristo bandia hayalingani na Maandiko. Mibaraka yake ameitoa kwa waabudu mnyama na sanamu yake, watu ambao watamwagiwa ghadhabu ya Mungu isiyo na huruma, kama Biblia isemavyo.TU 304.2

  Zaidi ya hayo, shetani hataruhusiwa kuigiza kabisa jinsi Kristo atakavyokuja. Mwokozi amewaonya watu wake kuhusu sehemu hii, ya udanganyifu. Amesema “kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa, na maajabu wapate kuwapoteza, kama yumkini, hata wateule … Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yuko nyumbani msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu”. Mat. 23:24-27. Soma pia Mathayo 25:31; ufunuo 1:7; 1Thes. 4:16-17. Kuja kwa jinsi hii, hakuna uwezekano wa kukuigiza. Kutaonekana katika ulimwengu mzima.TU 304.3

  Wanafunzi wa kweli wa Biblia tu, waliopokea upendo wa kweli ndio watakingwa na madanganyo haya makuu, yatakayoukumba ulimwengu. Ushuhuda wa Biblia pekee ndio utakaompinga mdanganyaji katika hila zake. Je, watu wa Mungu sasa wameimarika katika Neno la Mungu, kwamba hawatatikiswa na kuangukia mbali katika madanganyo? Je, katika matatizo kama hayo wataambatana na Biblia tu?TU 304.4

  Kwa vile amri itakavyotolewa na makanisa ya kikristo mahali mahali ili kuwapinga washika sabato, serikali haitawalinda, ila itawaacha kusudi watendwe mabaya na wale wanaotaka kuwatenda vibaya. Ndipo watu wa Mungu watakimbia kutoka mijini na vijijini, na kujikusanya vikundi vikundi, wakiishi mahali pa shida huko nyikani. Wengi watapata makao mapangoni mwa milima, sawa kama wakristo wa mabonde ya Piedmonti. Lakini wengi sana wa mataifa yote na wa kabali zote, watu wakuu na wadogo, matajiri na maskini weusi na weupe watatupwa katika vifungo vibaya sana. Wapenzi wa Mungu watapitia wakati mgumu sana, wakifungwa katika magereza, wakitajwa kuuawa, wakionekana kuwa watakufa katika giza magerezani.TU 305.1

  Je, Bwana atawasahau watu wake katika wakati wa dhiki kama hiyo? Je, alimsahau Nuhu mwaminifu au Lutu, Yusufu, Eliya, Yeremia au Danieli? Ingawa adui zao wawatupe magerezani, hata hivo kuta za magereza haziwezi kuwatenganisha na mbingu, wala kutenga roho zao na Kristo. Malaika watawazuru katika magereza ukiwa penye giza patang'azwa na nuru ya mbinguni kama ile iliyong'ara pale Paulo na Sila walipokuwa wakifungiwa, na kuimba katika mji wa Filipi.TU 305.2

  Hukumu za Mungu zitawaangukia wale waliokuwa wakitaka kuangamiza watu wake. Kwa Mungu, kutoa mapigo ni jambo geni. Isaya 28:21. Soma pia Ezekieli 33:11. Bwana ni “mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli… mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi” Hata hivyo “hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe” Kutoka 34:6-7; Nahumu 1:3. Taifa ambalo amelivumilia muda mrefu, na limekijaza kikombe cha uovu, mwishowe litakinywea kikombe cha ghadhabu ya Mungu isiyokuwa na huruma.TU 305.3

  Kristo amalizapo maombezi yake katika patakatifu pa mbinguni, ghadhabu yake isiyochanganyikana na huruma itawakabili wote waabuduo mnyama, itamwagwa. Mapigo ya Misri yalikuwa sawa na ghadhabu ya Mungu itakayomwagwa ulimwenguni, ila itakuwa kali zaidi. Ghadhabu hii itamwagwa kwa muda mfupi kabla ya ukombozi wa watu wa Mungu. Mwandishi wa Ufunuo asema, “pakawa na jipu baya, bovu, juu ya watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake” “Basi ikawa damu kama damu ya mfu”.TU 305.4

  “Na mito, na chemichemi za maji zikawa damu…. Malaika akatangaza, wewe u mwenye haki …. Ee, Bwana… Kwa kuwa umehukumu hivi... Kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na manabii wako, nawe umewapa wainywe; nao wamestahili” ufunuo 16:2-6, 8-9. Kwa kuwahukumia kifo watu wa Mungu, wamejipatia hatia ya damu yao; kana kwamba wameimwaga kwa mikono yao. Kristo alisema kuhusu Wayahudi wa siku zake, kuwa walikuwa na hatia ya damu ya watakatifu wote, tangu ziku za Habili (Mathayo 23:34-36) maana hata wao wanayo roho ile ile ya uuaji wa manabii.TU 305.5

  Pigo litakalofuata litatolewa kwa jua. Jua litapewa uwezo wa kuwaunguza watu kwa joto. Nabii asema kuhusu wakati huo wa kutisha: “maana mavuno ya mashamba yamepotea” ….“Mizabibu imesinyaa, mtini nao umeiva, nao mkomamanga, na mtende, na mtofaa, naam, miti yote ya mashamba imekauka, maana furaha imekauka katika wanadamu. Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe wamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam makundi ya kondoo yamepata mateso. Vijito vya maji vimekauka, na moto umeyateketeza malisho nyikani.” Yel. 1:11-12, 18-20.TU 306.1

  Mapigo haya hayatapiga ulimwengu wote, lakini yatakuwa mabaya sana sana kwa wale watakaoyapata. Mapigo yote ya Mungu yaliyotokea kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema, yamekuwa yenye huruma ndani yake. Damu ya Kristo imemkinga mwenye dhambi asipate adhabu inayostahili hali yake. Lakini katika hukumu ya mwisho, mapigo ya adhabu ya Mungu hayatakuwa na huruma. Watu watatafuta kificho cha Mungu waliyemdharau.TU 306.2

  Wakati watakaposumbuka kuona dhiki, wakitafuta chakula, watu wa Mungu hawataachwa wapotee. Malaika watawaletea mahitaji yao. “atapewa chakula chake maji yake hayatakoma” “Mimi Bwana nitawasikia, mimi Mungu wa Israeli sitawaacha” Isaya 33:16; 41:17.TU 306.3

  Kwa kibinadamu itaonekana kuwa karibuni watu wa Mungu watamwaga damu yao, yaani watauawa, kama wafia dini wengine waliowatangulia. Ni kitambo cha utisho wenye uchungu. Waovu wanashangilia na kusema Je, imani yenu iko wapi. Mbona Mungu hakuwaokoa mikononi mwetu, iwapo kweli ninyi ni watu wake? Lakini watu wa Mungu wanakumbuka Yesu alivyokufa mslabani. Kwa hiyo wanaendelea kushuhudiana na Mungu tu kama Yakobo.TU 306.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents