Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  40/Watu wa Mungu Wakombolewa

  Wakati ulinzi wa kibinadamu wa kisheria utakapoondolewa kwa watu wenye kuiheshimu sheria ya Mungu ndipo kutakuwa miondoko kadhaa katika nchi mbalimbali ya kuwaangamiza. Wakati unapokaribia wa kuwaangamiza, kama ilivyoamuriwa, watu wataazimu kuwavamia usiku mmoja ili kuwanyamazisha kabisa.TU 309.1

  Watu wa Mungu, wengine wamo magerezani, wengine wamo misituni milimani, wanaendelea kumsihi Mungu awahifadhi. Watu wenye silaha, wakihimizwa na malaika wa shetani, wanajitayarisha kuwaangamizia mbali. Sasa katika muda wa wasiwasi mno, Mungu ataingilia kati. “Mtakuwa na wimbo kama vile wakati wa usiku kama vile mtu aendapo … katika mlima wa Bwana, aliye mwamba wa Israeli. Naye Bwana atawafanya watu kusikia sauti yake ya utukufu, naye atawaonyesha jinsi mkono wake ushukavyo, na ghadhabu ya hasira yake na mwako wa moto ulao, pamoja na dhoruba, na tufani, na mvua ya mawe ya barafu” isaya 30:29-30.TU 309.2

  Makundi ya watu waovu yako karibu kuwavamia wana wa Mungu, wakati giza kuu, na kuu kabisa kuliko usiku lilifunika dunia. Kisha upinde wa mvua ukatanda mbinguni na ukaonekana kama upinde huo unawazungushia hawa wana wa Mungu. Kundi la waovu linazubaa. Kusudi lao limesahaulika, sasa wanakodolea macho juu ya ishara ya agano la Mungu, na wanataka wafunikwe wasione mng'aro huo.TU 309.3

  Kwa watu wa Mungu sauti ilisikika ikisema, “Tazamameni juu” Wakatazama juu wakauona utukufu wa Mungu na Mwana Kondoo katika kiti cha enzi, kama Stefano alivyoona. Matendo 7:55-56. Walizitambua alama za misumari, ambazo ni alama za kujidhili kwake. Kisha wakasikia neno “nataka hao ulionipa wawe pamoja nami” Yohana 17:24. Sauti ilisikika ikisema, “Wanakuja, wametakaswa, hawana waa lolote, wala uchafu! Wameshika neno la uvumilivu wangu”.TU 309.4

  Kwenye usiku wa manane Mungu aonyesha uwezo wake wa ajili ya kuwaokoa watu wake. Jua latokea liking'aa kwa nguvu. Maajabu na ishara vyafuata. Waovu wakaangalia kwa hofu kuu juu ya mambo hayo, wakati wateule wanaona kuwa hizo ndizo ishara za ukombozi wao. Katikati ya mbingu zilizokasirika, kunatokea nafasi wazi yenye utukufu usioelezeka, ambako sauti ya Mungu inatokea ikinguruma kama maporomoko ya maji, ikisema, “Imekwisha kuwa!” Ufunuo 16:17.TU 309.5

  Sauti hiyo hutetemesha mbingu na nchi. Litatokea tetemeko la nchi. “Kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi, hapakuwa namna ile”. Ufunuo 16:18. Miamba mikubwa ikatupwa huku na huko juu ya nchi. Bahari ikasukasuka kwa fujo na ghasia. Kukasikika sauti ya kilio na mvumo wa tufani kama sauti ya mashetani. Uso wa nchi ukavunjikavunjika. Msingi wake ukaonekana kana kwamba umeng'oka. Bandari kuu zilizofananishwa na Sodoma kwa uchafu na ufisadi wake, zikazamishwa na bahari yenye msukosuko. Babeli mkuu, amekumbukwa mbele za Mungu, ampe kikombe cha ghadhabu ya uchafu wake. Ufunuo 16:19. Mvua ya mawe makubwa inafanya kazi yake ya kuponda watu. Miji mikuu yenye kiburi inaangushwa chini. Majumba makubwa, ambamo wakuu na matajiri walifanyia anasa zao yakabomolewa machoni mwao. Magereza yakapasuliwa na watu wa Mungu waliofungiwa huko wakatoka.TU 310.1

  “Makaburi yakafunguliwa, na wengi wao waliolala mavumbini... wakaamka, wengine wapate uzima wa milele, na wengine wapate aibu na kudharauliwa milele”TU 310.2

  “Na wale waliomchoma Kristo, waliokuwa wakimdhihaki na kuchekelea kifo chake cha uchungu mkuu” “na wale waliokuwa wapingaji wakuu wa ukweli, watafufuliwa wapate kuona heshima watakayopewa waaminifu na watiifu wa sheria ya Mungu” Dan. 12:2 Ufu 1:7.TU 310.3

  Umeme mkali unametameta ukizunguka nchi, ukiwa kama mwali wa moto. Juu ya ngurumo za ajabu, sauti, za sirisiri na masikitiko zikitangaza ajali ya waovu. Wale waliokuwa wenye majivuno na wapinzani wakuu, wakatili kwa watumishi wa Mungu, sasa wanagwaya kwa hofu. Mashetani wanatetemeka, wakati watu wanaomba msamaha.TU 310.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents