Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utangulizi

  Kufunua Kifuniko Ili Kuona Mambo Yajayo*

  Kabla dhambi haijaingia ulimwenguni Adamu alifurahia maongezi pamoja na Muumba wake; lakini tangu watu walipojitenga wenyewe na Mungu wao kwa ajili ya uasi wanadamu wamekatwa kabisa na uhusiano wao umevunjika. Walakini kwa njia ya mpango wa wokovu njia imefunguliwa tena ambayo itawarudisha wanadamu katika ushirikiano na mbingu. Mungu amewasiliana na wanadamu kawa njia ya Roho Wake, na nuru ya Mungu imetolewa ulimwenguni kwa ajili ya ufunuo kwa watumishi waliochaguliwa: “Watakatifu wa Mungu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” 2Petro 1:21.TU iii.1

  Katika muda wa miaka 2500 ya kwanza ya historia ya wanadamu hapakuwako na maandiko yo yote yaliyofunuliwa. Wale waliofundishwa na Mungu walipitisha elimu hiyo kwa wengine, na ikapitishwa vivyo hivyo toka kwa baba mpaka kwa mwana kufuatana na vizazi. Matayarisho ya kutumia maandiko yalianzia kwa wakati wa Musa. Maandiko matakatifu yaliunganishwa pamoja katika kitabu kitakatifu. Kazi hii iliendelea muda mrefu wa miaka 1600 — tangu Musa aliyeandika historia ya uumbaji na sheria, mpaka Yohana, mwandishi wa kweli tukufu za Injili.TU iii.2

  Biblia inamtaja Mungu kuwa mwandishi wake, lakini iliandikwa kwa mikono ya wanadamu, na kwa namna mbalimbali katika vitabu vyake huonesha tabia ya waandishi. Ukweli ulioandikwa humo wote una “Pumzi ya Mungu” (2Tim. 3:16) Lakini ukweli wote unaelezwa katika lugha ya kibinadamu, yaani maneno ya watu. Mungu Mwenyenzi kwa njia ya roho Mtakatifu aliwavuvia watumishi wake katika mawazo yao na katika mioyo yao. Aliwapa ndoto na njozi, na mifano na tarakimu, na wote waliopewa mambo hayo waliyakusanya wakayandika kwa kutumia maneno ya lugha ya kibinadamu.TU iii.3

  Vitabu vya Biblia vilivyoandikwa nyakati mbalimbali na watu tofauti tofauti hali zote, na kwa kazi mbalimbali, huleta haki pana sana na aina ya uandishi tofauti lakini ujumbe ule ule. Kwa mtu mzembe ambaye anasoma juu juu tu huonekana kwamba Biblia inajipinga yenyewe, lakini kwa msomaji makini ataona kuwa Biblia haipingani hata kidogo.TU iii.4

  Kwa jinsi ilivyoandikwa na waandishi wetu mbalimbali kweli imeletwa kwa aina mbalimbali. Mwandishi mmoja anakazia hasa jambo fulani, hushikilia viini vinavyohusiana na uzoefu wake na mwingine anasisitizia jambo jingine, na kila mmoja kwa kuongozwa na roho mtakatifu ujumbe wao wauletao huwafaa watu wa hali zote.TU iii.5

  Mungu anapenda kwamba ukweli wake utangazwe ulimwe-nguni kwa njia ya wanadamu, na yeye Mwenyewe amewawezesha kufanya kazi hii kwa Roho Wake Mtakatifu. Aliwaongoza mawazo yao yapi ya kusema na yapi ya kuandika. Ujumbe wa thamani umekabidhiwa kwa vyombo vya duniani, lakini ni ujumbe wa mbinguni, na kweli iliyofunuliwa huunganishwa na kukamilika ili kufaa mahitaji ya wanadamu katika hali zote za maisha yao. Maneno ya ushuhuda hutolewa katika hali zote za maisha yao. Maneno ya ushuhuda hutolea katika lugha hafifu ya binadamu, lakini ni ushuhuda wa Mungu na wenye kuuamini ataona uwezo wa Mungu ndani yake umejaa neema na kweli. Katika neno lake Mungu ametoa mambo yote ya lazima kwa wokovu wa wanadamu. Maandiko matakatifu budi yapokelewe kama mwongozo halisi wa ufunuo wa mapenzi ya Mungu. Maandiko Matakatifu ndiyo kipimo kamili cha tabia na mafundisho.TU iv.1

  “Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” 2Tim. 3:16-17.TU iv.2

  Lakini alipokuwa Mungu amemfunulia mwanadamu mapenzi yake kwa njia ya neno lake, si kwamba amekomaa kuwaongoza watu kwa Roho Wake Mtakatifu. Kinyume cha huyo Roho Mtakatifu aliahidiwa ili apate kulitafsiri neno la Mungu kwa watu, ili wapate kuelewa na kushika mafundisho yake. Kwa kuwa roho Mtakatifu ndiye aliyewaongoza waandishi wa Biblia, hivyo haiwezekani kwa Roho Mtakatifu kupingana na hilo Neno.TU iv.3

  Roho hakutolewa ili kuchukua nafasi ya Biblia. Kwa maana Maandiko yanasema wazi kwamba, neno la Mungu ndilo kipimo cha kupimia mafundisho yote ya Imani zote. Mtume Yohana asema, “Msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu. Kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”. 1Yohana 4:1 na Isaya naye anasema, “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawa sawa na neno hili, bila shaka kwa hao hamna asubuhi”. Isaya 8:20.TU iv.4

  Shutumu kubwa limetupwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu kwa njia ya au wanaotangatanga huku na huku wakidai kwamba wanaongozwa na Roho Mtakatifu, wakisema kwamba hakuna haja ya kuongozwa na neno la Mungu. Wanatawaliwa na hali ya kujisikia msisimko kwamba hiyo ndiyo sauti ya Roho katika mioyo yao. Lakini hali hiyo inayowatawala siyo Roho wa Mungu. Kule kujisikia msisimko kukifuatwa huishia katika machafuko, udanganyifu na uharibifu. Hali hiyo huendeleza tu kazi ya mwovu. Kwa kuwa kazi ya Roho Mtakatifu ni muhimu sana katika kanisa la Kristo, ni makusudi ya Shetani kubuni mbinu za uongo kwa njia ya wakorofi wanaotangatanga na kujipendekeza kwamba wanaongozwa na Roho ili kuchafua kazi ya Roho na kuwafanya watu wa Mungu wasijali maandiko ambayo ndiyo njia iliyowekwa na Bwana mwenyewe.TU v.1

  Pamoja na neno la Mungu Roho Mtakatifu ataendelea na kazi yake katika muda wote wa ujumbe wa Injili. Wakati ule ambapo Maandiko ya Agano la kale na Agano Jipya yaliyotolewa, Roho Mtakatifu hakuacha kuwasiliana na watu na kuwavuvia, mbali na alivyowaongoza katika kazi ya kuunganisha maandiko matakatifu katika kitabu. Biblia yenyewe inasema, jinsi watu walivyopata maonyo, kemeo mashauri na maongozi katika kazi ya kuunga Biblia kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hata manabii kadhaa wametajwa katika vizazi mbalimbali ambao maneno yao hayakuandikwa. Vivyo hivyo baada ya mkusanyo wa maandiko Matakatifu na kuungwa katika kitabu, Roho Mtakatifu aliendelea na kazi yake ya kuwaelimisha, kuwaonya na kuwafariji watoto wa Mungu.TU v.2

  Yesu aliwaahidi wanafunzi wake. “Msaidizi huyu Roho Mtakatifu ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha, yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia” “….. na mambo yajayo atawapasha habari zake, atawaongoza katika kweli yote” Yoh. 14:26; 16:13. Maandiko Matakatifu yanaeleza wazi kwamba ahadi hizi ambazo hazikukomea katika siku za mitume tu, zinaendelea katika kanisa la Kristo katika siku za mitume tu, zinaendelea katika kanisa la Kristo katika vizazi vyote. Mwokozi anawahakikisha wafuasi wake. “Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” Mathayo 28:20. Na Paulo asema kwamba karama ya maono ya Roho Mtakatifu vitakuwamo kanisani. “Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa Imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”. Waefeso 4:12-13.TU v.3

  Kwa waumini wa Efeso Mtume aliomba, “Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa Utukufu, awape ninyi Roho ya Hekima na ya Ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la wito wake…. Na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadri ya utendaji wa nguvu za uweza wake.” Waefeso 1:17-19. Huduma ya Roho Mtakatifu katika kuelimisha, na kuwajulisha watu mambo ya Mungu kwa njia ya neno lake ndiyo mibaraka ambayo Paulo aliwatakia waumini wa kanisa la Efeso.TU vi.1

  Baada ya matokeo ya ajabu ya siku ya pentekoste, Petro aliwasihi watu watubu na kubatizwa kwa jina la Kristo, kwa ajili ya ondoleo la dhambi. “Nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtaktifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie” Matendo 2:38-39.TU vi.2

  Katika kuunganisha na siku kuu ya Mungu, Bwana kwa njia ya nabii Yoeli aliahidi maonyesho ya Roho Mtakatifu. Yoel 2:28. Unabii huu ulitimia sehemu katika siku ya Pentekoste; lakini utatimia kikamilifu wakati wa neema kuu ya Mungu itakayoonekana wakati wa kufunga kazi ya injili.TU vi.3

  Mapambano makali baina ya wema na uovu yataendelea na kuzidi mpaka mwisho kabisa. Katika vizazi vyote hasira ya Shetani imeonekana ikipinga Kanisa la Mungu, na Mungu amewapa watu wake neema ili waweze kupingana na maovu hayo. Wakati mitume wa Kristo walipopaswa kueneza ujumbe mahali mahali ulimwenguni Mungu aliwajalia uwezo kwa neema yake, walimwagiwa Roho Mtakatifu na uwezo mwingi. Lakini kadiri kanisa linapokaribia mwisho, ili liokolewe, shetani atajitahidi sana kwa nguvu kulipinga. Ameshuka chini mwenye ghadhabu kuu, kwa kuwa anajua kuwa ana muda mdogo sana. Ufunuo 12:12. Atafanya kazi akitumia ishara na ajabu za uongo. 2Thesalonike 2:9. Kwa muda wa miaka 6,000 ibilisi huyu ambaye hapo kwanza alikuwa malaika Mkuu wa Mungu, amejitahidi kudanyanya ulimwengu kwa kila njia ya kuuangamiza. Ujanja wake wote na udanganyifu wa kishetani na ukatili na kila hali vyote vitatumiwa kuwapinga watu wa Mungu katika shindano la mwisho, na wakati huu wa hatari kuu, watu wa Mungu watatoa maonyo ya mwisho katika ulimwengu, kuhusu kuja kwa Yesu mara ya pili. Watu lazima watayarishwe ili kusimama mbele ya Kristo pasipo “mawaa wala kunyanzi”. 2Petro 3:14. Wakati huu neema ya Mungu itakayohitajiwa haitapungua kwa ile iliyotolewa siku ya Pentekoste, siku za mitume.TU vi.4

  Mwandishi wa kitabu hiki amefunuliwa mapambano haya baina ya wema na uovu na Roho Mtakatifu. Wakati kwa wakati ameruhusiwa kuona maendeleo ya shindano hili ambalo limeendelea kwa vizazi vyote. Kristo ambaye ni mkuu wa uzima ndiye mwanzilishi wa wokovu wetu. Shetani, ambaye ni mkuu wa giza ndiye mwanzilishi wa dhambi, na ndiye aliyekuwa muasi wa kwanza wa sheria ya Mungu Takatifu. Uadui wa Shetani juu ya Kristo umeonekana dhahiri kwa wafuasi wake. Uadui ule ule uliokuwa wa kupinga kanuni za Mungu, njia ile ile ya udanganyifu ambayo hufanya kosa lionekane kuwa ni kweli, na kufanya sheria za watu kuwa bora kuliko za Mungu, kwa njia hiyo watu wameongozwa kuabudu kiumbe badala ya Mwumbaji, hali hiyo ikifuatiliwa inakwenda katika Historia yetu iliyopita. Juhudi ya shetani ya kumsema Mungu vibaya na kuharibu tabia yake, ili watu wamwelewe Mungu vibaya, wamwone kuwa ni katili wala hana upendo wowote, huwafanya watu wamwogope na kujaribu kuepukana na matakwa yake kadiri iwezekanavyo. Hali hiyo shetani ameitumia katika vizazi vyote. Hali hiyo ilionekana siku za Wazee na Manabii, Mitume na Wafia dini na za Watengenezaji wa kanisa.TU vii.1

  Katika pambano kuu la mwisho, shetani atatumia njia zile zile hali ile ile, na namna ile ile ilivyokuwa nyakati za nyuma. Jinsi ilivyokuwa, ndivyo itakavyokuwa, isipokuwa tu shindano la kutisha, ambalo ulimwengu haujaliona. Madanganyo ya shetani yatakuwa ya ujanja mno na werevu mwingi. Mashambulio yake yatakuwa makali sana. Kama ikiwezekana yawapoteze hata wateule. Marko 13:22.TU vii.2

  Jinsi Roho wa Mungu alivyonifunulia ukweli mkuu wa neno lake, na mambo yaliyopita na yale yajayo, nimeagizwa kuwajulisha wengine mambo haya, yaliyofunuliwa kwangu, kufuatilia historia ya mapambano yaliyokuwa hapo katika vizazi vya nyumba na yalivyo sasa na jinsi yakatakvyokuwa wakati ujao. Katika kushughulika na jambo hili nimejitahidi kuchagua na kupanga pamoja matokeo mbalimbali katika historia ya kanisa, ili kuona jinsi ukweli ulivyofunuliwa katika nyakati tofauti, na kutangazwa ulimwenguni, na jinsi ukweli huo ulivyochochea ghadhabu ya Shetani na uadui wa kanisa liupendalo ulimwengu ambao umetangazwa na watu ambao “hawakuthamini maisha yao hata kufa”TU vii.3

  Katika maandishi haya tutaona kivuli cha mapambano yanayotukabili. Kuhusu mambo haya, katika nuru ya Neno la Mungu na uvuvio wa Roho tutaona jinsi mbinu za mwovu zinavyopangwa, pamoja na hatari, ambazo lazima ziepukwe na wale ambao watakutwa “bila mawaa” wakati wa kurudi kwake Bwana.TU viii.1

  Matokeo makuu yaliyokuwa wakati wa matengenezo yamekuwa historia tu iliyopita ambayo inajulikana sana na kukubaliwa na makanisa yote ya kiprotestanti. Kuna ukweli usioweza kukanushwa. Historia hii nimesimulia kifupi tu, katika kitabu ambacho kimefupishwa, ambacho ukweli umefupishwa kwa ufahamu wa matumizi yake. Mahali pengine mtunzi au mwandishi wa historia ametoa maelezo kamili au pengine inapolazimu maneno yake yamenakiliwa, pengine imeachwa tu kama ilivyosimuliwa. Katika kusimulia mambo ya hao watengenezaji wa kanisa katika siku zetu, matumizi yale yale kutoka katika maandiko yao yametajwa.TU viii.2

  Siyo kusudi la kitabu hiki kuleta ukweli mpya kuhusu mapambano haya ya zamani, ila kuleta kanuni za kweli kuhusu matokeo yajayo. Lakini kukumbusha sehemu iliyopita huonekana kuna umuhimu, maana humulika hali ya siku za mbele, kwa wale watakaopambana na hali hiyo kama watengeneza dini walivyofanya, kushuhudia na kutetea neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo.TU viii.3

  Kitabu hiki hasa kusudi lake ni kufunua pambano kali kati ya kweli na uongo, kuonesha hila za Shetani, na njia ya kufaulu kuzipinga, kuonesha njia ya kutatua tatizo la uovu, kufunua upendo wa Mungu na haki yake jinsi anavyochukuliana na viumbe vyake, na kuonesha sheria ya Mungu isiyobadilika. Ili kwa kukisoma watu waweze kuokolewa kutoka katika nguvu za giza ili washiriki urithi wa watakatifu. Sifa kwake yeye aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ndiyo sala ya dhati ya mwandishi.TU ix.1

  E.G.WhiteTU ix.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents