Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Waliokombolewa Katika Utukufu

  Katika vizazi vyote wateule wa Mwokozi wamekuwa wakitembea katika njia nyembamba. Walitakiwa katika tanuru la mateso. Kwa ajili ya Kristo walivumilia chuki masingizio, masengenyo, kujikana, na machungu mengi. Wamejifunza ubaya wa dhambi, nguvu ya dhambi, na hatia ya dhambi, na matokeo ya dhambi. Wameiona katika hali ya kuichukia. Kuifahamu dhabihu ya Mwokozi kwa ajili yao, kumwafanya kuwa wanyenyekevu na wapole. Wamependa sana kwa sababu wamesamehewa mengi Luka 7:47. Kwa kuwa wamekuwa washiriki wa mateso ya Kristo, wamestahili pia kuwa washiriki wa utukufu wake.TU 316.2

  Warithi wa Mungu wanatoka mahali hafifu, vijumba vya ovyo, gerezani, mapangoni, milimani, jangwani mwituni. Ni watu wa dhiki tu daima. Waliteswa wengi walilala makaburini katika hali ya dhiki na fedheha, kwa sababu walikataa kusalimu amri kwa shetani. Sasa hawana dhiki tena wala masumbuko. Hivyo sasa wanasimama katika furaha isiyosemekana, na kuvaa mavazi ya utukufu. Wanavaa taji tukufu, ambayo kamwe havikuvaliwa na mfalme ye yote duniani. Mfalme wa utukufu amefuta machozi yote katika macho yao. Wanaimba tu nyimbo za kusifu safi na tamu. Mbingu inajaa na nyimbo zikisema “wokovu una Mungu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwanakondoo” na wote wanaitikia wakisema “Amina, Baraka, na utukufu, na hekima na shukrani na heshima, na uwezo na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele” ufunuo 7:10-12.TU 316.3

  Katika maisha haya tunaweza tu kuanza kufahamu mpango wa wokovu. Kwa akili yetu ndogo tunaweza kuelewa mambo ya aibu na ya utukufu, uzima na mauti, haki na rehema ambayo hukutania msalabani; lakini kwa ajili ya uhafifu wetu tunashindwa kuelewa mambo yayo hayo katika umuhimu wake. Urefu, na upana na kwenda juu na kina cha upendo wa ukombozi tunavifahamu kidogo sana kigizagiza. Mpango wa wokovu hautafahamika kamili hata kama waliokombolewa watafika huko na kuona mambo waziwazi; na kujua kama wanavyojulikana, lakini kwa maisha ya milele na milele, kweli mpya, mpya zitaendelea kufunuliwa kwa watu wenye mawazo ya utambuzi kamili, ambao watakuwa wakishangaa na kujifunza wakati wote. Ijapokuwa masikitiko na magonjwa na uchovu pamoja na majaribu ya dunia vimekwisha, na laana imeondolewa, watu wa Mungu watakuwa na akili timamu ya kujua kwa kweli kila kilichogharimisha wokovu wao.TU 316.4

  Msalaba ndio utakuwa kiini cha elimu ya kujifunza na wimbo wa kuimba milele na milele zote. Katika Kristo mwenye utukufu, watamwona jinsi alivyosulubishwa. Kamwe haitasahauliwa kuwa mkuu wa utukufu mbinguni alijinyenyekeza ili kusudi apate kuwainua walioanguka dhambini. Kwamba alichukua maovu na masikitiko yote, na uso wa Baba yake alificha usimwelekee Yesu, na ole wa ulimwengu mzima ukamkalia mpaka roho yake ikavunjika na kufa. Mwumbaji wa ulimwengu aliacha tukufu wake ili kumwokoa mpotevu. Upendo huu wa Yesu kwa binadamu, kamwe hautasahaulika katika malimwengu yote. Mataifa ya waliookoka watakapomwangalia Mwokozi, na kujua kuwa ufalme wake hauna kikomo, basi wanapaza sauti wakimba: “Anayestahili ni Mwanakondoo, aliyechinjwa akatukomboa kwa damu yake, na kutufanya wana wa Mungu”TU 317.1

  Siri ya msalaba inafunua siri zote. Itaonekana wazi kuwa mwenyenzi Mungu mwenye hekima yote asingebuni njia nyingine ya kumwokoa mwanadamu isipokuwa ni hiyo ya kujitoa kwa mwana wake. Matokeo ya kujitoa huku ni kujaza watu katika dunia, ambao waishio milele. Hiyo ndiyo thamani ya roho, ambayo ililipiwa gharama hiyo na Baba aliridhika nayo. Na Kristo aonapo matunda ya kafara yake kuu ataridhika.TU 317.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents