Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  41/Dunia Katika Maangamizi

  Wakati sauti ya Mungu itakapofungulia watu wake, kutakuwa na mwamko wa kutisha kwa wale walioshindwa, katika mapambano haya ya maisha. Wakipofushwa na madanganyo ya shetani, matajiri wakijivuna juu ya wale waliokuwa na mali kama zao. Lakini hawakuwajali maskini, wenye njaa, walio uchi, wala hawakutenda matendo ya haki, huruma na upendo. Sasa vitu vyao vyote wamenyag'anywa wameachwa fukara. Wakaangalia kwa hofu kuu uangamivu wa sanamu zao ambavyo walivifanyia miungu yao. Waliuza roho zao katika furaha na anasa za dunia. Maisha yao yamekuwa katika hali ya ufukara. Mali walizochuma katika maisha yote zimeyeyuka kwa kitambo. Matajiri wanaombeleza, kwa ajili ya maangamizi ya majumba yao makubwa. Mtawanyiko wa dhahabu na fedha zao. Wana hofu kuangamia na sanamu zao. Waovu wanaomboleza kwa sababu matokeo yamekuwa hivyo, wala hawakutubu.TU 318.1

  Mchungaji aliyeacha ukweli ili apendwe na watu anafahamu sasa kuwa mafundisho yake yalikuwa na mvuto mbaya. Kila mstari ulioandikwa na kila neno lililonenwa ambalo liliwafanya watu watulie katika ngome ya uongo, lilikuwa mbegu iliyopandwa, sasa wanaona mavuno yalivyo. Bwana asema “Ole wao wachungaji wanaoharibu kondoo za malisho yangu, na kuwatwawanya … Angalieni nitawapatiliza uovu wa matendo yenu.” “Mnemhuzunisha moyo wenye haki ya uongo, ambaye mimi sikumhuzunisha, na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya hata asigeuke na kuiacha njia yake mbaya” Yeremia 23:1-2; Eze.13:22.TU 318.2

  Wachungaji wa watu wao wanaona kuwa, kumbe walikuwa wamemwasi Mwenye sheria zote za haki, yaani Mungu. Walipoiacha sheria, wakafungua njia ya maasi yote, mapaka nchi ikawa ziwa la uharibifu. Lugha haitoshi kuelezea hali ya kutamani waovu waliyo nayo ya kupata uzima. Lakini saa wamepoteza milele, uzima wa milele.TU 318.3

  Watu wanashitakiana wao kwa wao kwamba wamekoseshwa mpaka wamepotea, lakini wote wakaelekeza matusi yao ya kuwalaani wachungaji ambao wamewakosesha.TU 318.4

  Wachungaji ambao walisema maneno laini (Isaya 30:10) ambayo yaliwafanya watu wajiepushe na sheria ya Mungu. Watainuka na kusema “Tumepotea, na ninyi ndio mliotukosesha” Mikono ile iiyokuwa ikiwasifu na kuwatukuza, sasa inawainukia ipate kuwaangamiza. Kila mahali palijaa mapigano na kumwaga damu!TU 318.5

  Mwana wa Mungu pamoja na wenyeji wa mbinguni wamekuwa wakipambana na uovu, huku wakiwamulikia, na kuwavuta watu ili watoke katika njia za uovu na kuelekea nuru ya uzima. Na sasa kila mtu ameamua upande wa kusimama. Waovu waliamua kuungana na shetani ili kushindana na Mungu. Kwa hiyo mapambano si ya shetani peke yake, bali ni wanadamu pia. “Bwana anayo mateto pamoja na mataifa”. Yeremia 25:31.TU 319.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents