Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Malaika wa Mauti

  Sasa malaika wa mauti anatoka, katika njozi ya Ezekieli akifananishwa na watu wenye silaha za kufisha. “Waueni kabisa, mzee, na kijana na msichana na watoto wachanga na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama, tena anzeni katika patakatifu pangu”. Basi wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba “waliodai kuwa waongozi wa watu” Eze. 9:6. Walinzi wa uongo ndio wa kwanza kuanguka. “Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao, ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunuka tena watu wake waliouawa”. “Mashaka makubwa yatokanayo kwa Bwana yatakuwa kati yao, na kila mmoja wao atakamata mkono wa jirani yake, na mkono wake utainuliwa ili kushindana na mkono wa jirani yake” Isaya 26:21; Zekaria 14:12-13.TU 319.2

  Mashindano yao ya kinyama, pamoja na mapigo ya Mungu yasiyochanganywa na huruma, wataanguka waovu, makuhani, wakuu, na watu kwa ujumla. “Na waliouawa na Bwana siku ile watakuwako, toka upande mmoja wa dunia na hata upande wa pili”. Yeremia 25:33.TU 319.3

  Katika kurudi kwake Kristo, waovu watauawa kwa mng'aro wa utukufu wake. Kristo anachukua watu wake mpaka katika jiji la Mungu. Nchi inabaki tupu bila wakaaji. “Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua na kuwatawanya wakaao ndani yake… Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana Bwana amenena neno hilo... Kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele. Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea.” Isaya 24:1,3,5-6.TU 319.4

  Dunia inaonekana kama jangwa. Miji imeharibiwa na tetemeko la nchi, miti imeng'oka, miamba na mawe makubwa yametawanyika kote. Mashindano makubwa yanaonyesha mahali milima ilipokuwa. Misingi yake imetoweka.TU 320.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents