Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  42/Amani ya Milele Mwisho wa Mapambano

  Mwisho wa miaka 1000 Kristo anarudi duniani akifuatana na waliokombolewa na jeshi la malaika. Anawaita waovu waliokufa waamke ili wapate malipo yao ya ajali. Wanatokea wengi sana wasiohesabika, kama mchanga wa pwani wakiwa na hali zao za maradhi na kifo. Tofauti kubwa na wale waliofufuliwa mara ya kwanza.TU 323.1

  Kila jicho linamwangalia Mwana wa Mungu jinsi alivyo mtukufu. Waovu wanapaza sauti kwa umoja wakisema, “Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana”. Mathayo 23:39. Hasemi hivyo kwa upendo, ila tu ukweli wa mambo unawalazimisha kusema hivyo bila kutaka. Jinsi waovu walivyokufa wakiwa na hali ya ukafiri, ndivyo watafufuka wakiwa na hali hiyo. Hakuna nafasi ya kurekebisha tabia zao.TU 323.2

  Nabii asema, “Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizietuni …. Nao mlima wa mizeituni utapasuka katikati yake” Zekaria 14:4. Mji wa Yerusalemu unaposhuka chini, kutoka mbinguni, utatua juu ya mahali palipotayarishwa na Kristo pamoja na watu wake na jeshi la malaika, wanaingia mjini.TU 323.3

  Wakati shetani alipofungwa asipate mtu wa kudanganya alikuwa katika hali mbaya sana, lakini sasa aonapo waovu wamefufuka jeshi kubwa, matumaini yake yanamrudia. Anakusudia kuendelea na mapambano tu, wala asisalimu amri. Atalipanga jeshi lake vema, maana wote hao ni waasi kama yeye, wako tayari kufanya kama apendavyo. Hajitaji kuwa yeye ni shetani, bali ajitaja kuwa mtawala wa ulimwengu kihalali. Anatumia hila zake ili kuwahadaa. Kwamba ni yeye mrithi wa ufalme ila ananyang'anywa haki yake kwa dhuluma. Anajidai kuwa yeye ni mkombozi, anao uwezo wa kushinda vita, kwamba uwezo wake ndio umewatoa makaburini. Shetani anawatia nguvu wote walio dhaifu, na kuwachochea kwa bidii ili wakauteke mji wa Mungu. Anaona jeshi kubwa la watu waliofufuka na kusema kuwa yeye kama kiongozi wao atashinda na kutwaa enzi yake.TU 323.4

  Katika jeshi hilo yamo majitu ya zamani yaliyoishi kabla ya gharika, majitu makubwa yenye akili na uwezo mwingi kimawazo, ambao walikuwa waasi waliosababisha gharika. Pia kulikuwamo na wafalme na majemadari wakuu ambao siku zao hawakushindwa vita kamwe. Watu hawa hawakubadilika, maana katika kifo hakuna kubadilika. Walipofufuka walikuja na hali yao ile ya vita na ukatili.TU 323.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents