Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Waasi watamkiwa Hukumu

  Kutawazwa kwa Kristo kunafanyika mbele ya wakaaji wambinguni na wenyeji wa duniani. Na sasa Kristo akikabidhiwa utukufu na nguvu, akiwa ndiye mfalme wa wafalme, awatamkia waovu ambao wameivunja sheria yake na kuwatesa wafuasi wake. “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vitabu vile, sawasawa na matendo yao”. Ufunuo 20:11-12.TU 325.2

  Macho ya Yesu yalipokuwa yakiwatazama waovu wao waliona kukumbuka kila aina ya dhambi waliyotenda maishani mwao. Wanaona mahali miguu yao ilipoteleza na kuacha njia nyofu. Wanaona majaribu yaliyowavuta na kuwaingiza dhambini kwa ajili ya tamaa. Wanaona jinsi walivyowadharau wajumbe wa Mungu pamoja na ujumbe wao. Ugumu wa ukaidi wa mioyo yao uliwazuia wasitubu, vyote vyaonekana kama vieandikwa kwa herufi za moto.TU 325.3

  Juu ya kiti cha enzi msalaba ulifunuliwa. Mfululizo wa maono kama picha ya mfululizo ikionyesha anguko la Adamu, na hatua zilizofuata katika mpango wa wokovu kuzaliwa kwa Mwokozi; maisha ya Mwokozi ya hali ya unyenyekevu na kujidhili, ubatizo wake kaitka mto wa Yordani, kuomba na kuanguka kwake jangwani, majaribu yake, huduma yake na huruma kwa wanadamu, ikionyesha mibaraka ya mbingu, kukesha kwake usiku katika kuomba mlimani, matendo yake mema yasiyo na kifani, matendo ya kihaini na usaliti aliyofanyiwa kufuata wema wake. Kuteseka kwake katika Getsemane akiona mzigo wa dhambi za ulimwengu ukimkalia. Kusalitiwa na kukamatwa kwake na kundi la wauaji usiku wa vitisho akiwa mikononi mwa makutano, mfungwa asiyekaidi ameachwa na wanafunzi wake; katika majumba ya hukumu na kwa wakuu katika jumba la hukumu la Pilato mbele ya mwoga Herode, kutukanwa, kudhihakiwa, kuteshwa kupita kiasi, na mwisho kusulubishwa msalabani. Yote yanaonekana wazi.TU 325.4

  Na sasa mbele ya majeshi yanayotetemeka yanafunuliwa maneno ya mwisho, mteswaji mvumilivu akikanyaga njia ya kwenda kalwari. Mfalme wa mbinguni akifa msalabani waandishi na makuhani huku wakimdhihaki. Mavumilivu yake makali wakati akifa. Giza laifunika dunia wakati akikata roho.TU 325.5

  Haya yote yalipoonekana shetani na wafuasi wake hawakuwa na la kusema, wala njia ya kujificha wasiyaone. Kila jambo lilimgonga sehemu aliyoifanya. Herode aliyechinja watoto wadogo wa Bethlehemu, Herodias mwenye hatia ya damu ya Yohana Mbatizaji, Pilato mwamuzi dhaifu, majeshi yaliyokuwa pale katika kumdhihaki Mwokozi, makundi ya waliopagawa waliopaza sauti zao na kusema, “Damu yake na iwe juu yetu na watoto wetu”. Wote hao walitafuta kutoroka, wasiweze. Wakati huo waliokombolewa, wakizitupa taji zao miguuni pa Mwokozi na kusema “Alikufa kwa ajili yangu”.TU 326.1

  Hapo yuko Nero, mkuu wa ukatili, anawaangalia wale aliowatesa katika hali ya unyama, watu hawa wametukuzwa kwa ajabu. Hata mamaye aliyemtia moyo wa ukatili kwa mfano wa mvuto wake, alikuwako akiyaona mazao ya matunda yake ya uasi uliotetemesha dunia.TU 326.2

  Mapapa na wakuu wao wapo hapo, waliokuwa wakijidai kuwa wao ndio mawakili wa Mungu duniani ambao walitumia ukatili kwa wana wa Mungu; ukatili wa kila aina; kufunga watu, kupiga kuchoma moto, na mateso ya namna namna. Mapapa waliojivuna majivuno makuu sana kuliko Mungu kiasi cha kutaka kubadili sheria ya Mungu. Sasa wamechelewa kugundua kuwa mwenyezi Mungu siyo wa kudhihakiwa kiasi hicho. Hawana udhuru wo wote sasa. Waasi wote wanashangaa pale kwa kujua kuwa walikuwa wanashindana na Mungu. Hawana la kujitetea. Tamko linatamkwa juu yao kuwa, watapata kifo cha milele kuwa ndiyo malipo yao. Waovu wanaona kuwa hayo ndiyo matunda ya uasi wao. Kwa hiyo wanapaza sauti kwa umoja wakisema, “Tumepotea mambo haya yote tungaliyapata, kama tungalijali maonyo! Tumebadili, furaha, amani, heshima, na uzima badala yake tumepata uharibifu aibu na kifo. Katika maisha yao walitangaza ‘hatumtaki Yesu atutawale’”.TU 326.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents