Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shetani Ashindwa

  Wakati waovu wakiangalia kutawazwa kwa mwana wa Mungu, waliona katika mikono yake alishika mbao mbili za amri zake ambazo walizidharau, kumbe ndio sheria ya serikali ya Mungu. Walishuhudia ibada ya waliokombolewa, ndipo waovu walisema, “Ni haki na za kweli njia zako, Ee, Bwana Mungu mwenyenzi” Wanasema hivyo huku wakianguka na kusujudu. Ufu. 15:3.TU 327.1

  Shetani alichanganyikiwa kiasi cha kufa ganzi. Aliyekuwa kerubi wa kusitiri, alikumbuka alikojikwaa na kuanguka, kutoka mahali pake pa heshima mbinguni. Alimwona malaika mwingine amesimama karibu na Baba, katika cheo alichokuwa nacho shetani. Akajua kuwa kama angalidumu kuwa mwaminifu angalikuwa na cheo chake.TU 327.2

  Alikumbuka jinsi alivyokuwa hapo zamani na heshima yake, amani aliyokuwa nayo. Alijikumbusha kazi yake katika ulimwengu na matokeo yake, kuwa ni chuki tu kati yao na uharibifu wa maisha. Akaona kuwa kilichomo ulimwenguni ni vita na kupinduana siku zote ni fujo na ghasia tu kila mahali. Akatafakari jinsi alivyojitahidi kupinga kazi ya Kristo. Alipoona matunda ya juhudi yake akaona kuwa hakuambulia chochote. Tena na tena katika vita vyake na Kristo amekuwa akishindwa kwa kila hatua, na kuombwa asalimu amri.TU 327.3

  Kusudi la uasi wake lilikuwa kuonyesha ufanisi wake zaidi ya serikali ya Mungu. Amewashawishi watu majeshi na majeshi kukubaliana naye katika mipango yake. Kwa muda wa miaka maelfu mkuu wa uovu huyu ameeneza uongo wake pote. Sasa wakati umefika ambao tabia halisi ya shetani itadhihirika wazi. Katika juhudi yake ya mwisho ya kumwondoa Kristo, kuangamiza watu wake, na kuuteka mji wa Mungu, mdanganyaji mkuu huyu amejidhihirisha kuwa ni mwongo, wala hana uwezo wa kufaulu lo lote kama alivyowaahidia wafuasi wake. Watu waliomfuata wanaona kuwa mambo yote, na mipango yake yote imekuwa bure.TU 327.4

  Shetani anaona kuwa uasi wake umemwondoa asifae kukaa mbinguni. Alijizoeza kushindana na Mungu; kwa hiyo uzuri wa mbingu ni fahari ya huko, kwake ingekuwa mateso matupu. Anainama chini na kukubali adhabu inayomstahili.TU 327.5

  Kila jambo la udanganyifu katika vita yake limedhihirika wazi, na ukweli umeonekana ulivyo. Matokeo ya kuacha sheria ya Mungu yameonekana yalivyo. Historia ya sheria ya Mungu yenye kumletea kila mtu raha na amani, inasimama kwa wote, ikiwa kama mashahidi wa kushuhudia kuwa Mungu anakusudia kuwaletea viumbe wake furaha daima. Viumbe vyote pia, vyenye kumtii na vilivyoasi, pamoja na shetani vinapaza sauti na kusema “ni za haki na za kweli njia zako, Ee Bwana, mfalme wa watakatifu”TU 327.6

  Wakati umefika ambapo Kristo atatukuzwa kupita majina yote. Kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake ya kuwaleta wana na binti katika utukufu, ilimfanya avumilie msalaba. Anawatazama waliokombolewa wakiwa na sura yake mwenyewe. Anaona mazao ya taabu ya nafsi yake na kuridhika. Isaya 53:11. Mbele ya waliokombolewa na waovu, anatamka, “Tazameni walionunuliwa kwa damu yangu! Kwa ajili yao niliteseka na kufa”TU 328.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents