Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ushindi wa Pendo la Mungu

  Hapo pendo la Mungu alilopanda mwenyewe mioyoni mwa watu litakamilika. Ushirikiano na viumbe vitakatifu, na umoja wa haki usio na kasoro, jamii yote ya mbinguni na ya duniani vitadumisha furaha ya milele iliyo kamili. Waefeso. 3:15. Hapo katika mawazo makamilifu tutaona maajabu ya uwezo wa Mungu wa kuumba, na siri za upendo wa ukombozi. Kila kiungo kitakuwa na kuendelea. Maarifa ya kujifunza hayatakua na kikomo. Mambo makuu ya ajabu yatafikiwa na hali ya juu ya mawazo na vifiko vyote vitafikiwa. Hata hivyo kutakuwa na mambo mengi ya ajabu ya kupekua. Kwa milele na milele kutakuwa na mafunzo yasiyo na mwisho wala hakuna kuchoka.TU 331.1

  Hazina zote za Mungu zitafunguliwa kwa wana wa Mungu waliokombolewa. Watatembea dunia nyingine bila kuwa na safari za kuchosha. Wana wa nchi hii wataingia katia ulimwengu wa wasiokuwa na dhambi na kushiriki maajabu ya elimu yao isiyokuwa na kasoro, ambayo wao wamekuwa nayo vizazi kwa vizazi.TU 331.2

  Wataangalia utukufu wa uumbaji bila kuwa na kiwi machoni. Na jua, nyota na sayari zote zikikizunguka kiti cha enzi.TU 331.3

  Kadiri miaka ya milele inavyokwenda, ndivyo ufunuo wa utukufu wa Mungu na Kristo utakavyofunuliwa kwa ajabu. Kwa kadri watu watakavyojifunza tabia ya Mungu ndivyo watazidi kumwabudu na kumpenda. Kadri Yesu anavyowafunulia siri za ukombozi wa vita kuu kati ya wema na ubaya ulivyoletwa na shetani, ndivyo watakavyozidi kumtukuza na kumtumikia, na kumwimbia kwa sauti za watu maelfu mara maelfu makumi, “Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari na vitu vyote vilivyo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi na yeye Mwana Kondoo hata milele na milele” Ufunuo 5:13TU 331.4

  Mapambano makuu yamekoma. Dhambi na wenye dhambi hakuna tena. Ulimwengu mzima sasa umeshafika. Umoja na ushirikiano ulio kamili kabisa umeenea ulimwenguni. Kutoka kwa Muumbaji hufurika uzima, nuru na furaha na kuenea mahali pote. Tangu kwa kitu kidogo mno mpaka kwa kikubwa kilinganacho na ulimwengu mzima, vitu vyote, vilivyo hai na visivyo hai, katika hali yote, hutangaza kuwa Mungu ni pendo.TU 331.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents