Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwepesi Kugundua Kosa.

  Wycliffe alikuwa mwepesi wa kugundua kosa na kulitaja wazi bila hofu, ingawa Rumi ililitetea. Wakati alipokuwa kasisi wa mfalme, Wycliffe alipinga kwa ushujaa malipo ya ushuru ambayo papa alidai kwa mfalme wa Uingereza. Majivuno ya papa kwamba anayo mamlaka hata kwa watawala wa nchi, yalikuwa kinyume cha haki na maadili.TU 31.1

  Madai ya papa yalichochea uchungu tu kwa watu, lakini mafundisho ya Wyclkiffe yalituliza watu. Kwa hiyo mfalme na mawaziri walikataa kulipa ushuru uliodaiwa na papa.TU 31.2

  Maskini waombaji wa watawa walijazana Uingereza, wakatia kasoro ukuu na umaarufu wa taifa. Maisha ya watawa ya kivivu, na hali ya kuombaomba mabarabarani hayakupunguza mapato ya watu tu, bali yalileta hali ya kufanya kazi ionekane kuwa duni. Vijana walipotoshwa na kuharibiwa. Wengine walijiingiza katika hali ya kuwa watawa, bila kuruhusiwa na wazazi wao, bila wao kujua kile wanachotenda. Hali hii ya ufedhuli, ilitokeza hali ya kinyama kabisa, kama Luther alivyoisema baadaye.TU 31.3

  Hata wanafunzi wa Chuo kikuu walishawishiwa na hawa watawa wakubali kufuata njia zao. Walipokwisha kunaswa ilikuwa vigumu kujinasua. Wazazi wengi walikataa kutuma watoto wao katika vyuo. Shule zilididimia, na ujinga ulistawi.TU 31.4

  Papa alikuwa amewapa watawa hawa uwezo au idhini ya kusikia maungamo ya watu na kuwasamehe makosa yao. Jambo hilo ni asili ya uovu mkuu. Watawa hawa walijitahidi sana kuachilia makosa ya kila namna kwa watu ili kuongeza mapato yao maana mambo yote yalifuatana na malipo. Zawadi zilizowastahili wagonjwa na maskini, ziliingia mifukoni wa hao watawa. Utajiri wa hao watawa uliongezeka na ustawi wao na hali yao ya kianasa ilifilisi taifa. Walakini watawa hao waliendelea kuwashikilia watu katika hali ya ushirikina, na kuwafanya waamini kuwa shughuli zote za kidini ni kutambua utawala wa papa na kuitukuza heshima ya watakatifu pamoja na kutoa vipaji kwa watawa. Kutenda mambo hayo kulitosha kuwafikisha mbinguni.TU 31.5

  Wycliffe akielewa vizuri, aligonga kwenye mzizi wa uovu, akieleza kuwa kawaida hiyo wanayoshikilia na kuiamini ni uongo mtupu, kwa hiyo lazima iachwe, na iondolewe. Mahubiri ya Wycliffe yaliamsha maswali na mawazo ya watu. Wengi walitaka kujua kama ni sawa kutafuta msamaha wa Mungu, au msamaha wa papa wa Rumi. “Watawa pamoja na maaskofu wa Rumi walisema, watu hawa (Wycliffe) wanatutafuna kama kanisa Mungu lazima atuokoe, au sivyo taifa litapotea” Watawa hao waombaji alisema kuwa wanafuata kielelezo cha Yesu na wanafunzi wake, ambao waliishi kwa kupata misaada ya upendo wa watu wasome Biblia ili waone ukweli ulivyo.TU 32.1

  Wycliffe alianza kuandika vijizuu na kuvitoa kwa watu ili kuyapinga madai ya watawa na kuwaeleza watu katika mafundisho ya Biblia. Hakuna njia nyingine ambayo Wyclife alitumia kubomoa ngome ya uongo iliyojengwa na Rumi kuwashikilia watu katika ujinga.TU 32.2

  Wycliffe aliyeitwa kutetea haki ya taji ya Uingereza kwa maingilio ya papa, alichaguliwa kuwa balozi wa Netherlands. Hapo Wycliffe alikutana na mapadri kutoka ufaransa, Italia na Spain. Alipata nafasi ya kuona ndani ya pazia yaliyokuwa yamefichika kwake alipokuwa Uingereza. Wajumbe hawa wa papa walionyesha tabia halisi. Baadaye alirudi Uingereza na bidii mpya ya kuendeleza mafundisho yake. Alitangaza kuwa huko Rumi ni majivuno na udanganyifu tupu ndivyo vilivyoko. Hivyo ndivyo mungu wao.TU 32.3

  Aliporudi uingereza Wycliffe aliwekwa na mfalme kuwa kasisi wa Lutterworth. Jambo hili lilithibitisha kuwa mfalme hakuchukizwa na mahubiri yake ya wazi. Mvuto wa Wycliffe ulienea katika nchi yote.TU 32.4

  Ngurumo za papa zilikuwa tayari kumlipukia Maazimio matatu ya papa yalitangazwa ili kumnyamazisha kimya huyo mzushi, mwalimu wa uongo.TU 32.5

  Matangazo ya papa yalipofika Uingereza yaliamuru kumfunga gerezani huyo mzushi.TU 32.6

  Ilionekana wazi kwamba Wycliffe karibu angeingia hatarini. Lakini yule aliyemwambia mtu wa zamani kuwa, “Usiogope…. Mimi ni ngao yako” Mwa. 15:1 Aliunyosha mkono wake kumlinda mtumishi wake. Kifo hakikumpata mtengenezaji wa mambo ya kanisa, bali kilimpata papa aliyeamuru kufungwa kwa Wycliffe.TU 33.1

  Kifo cha Gregory XI kilifuatiwa na uchunguzi wa mapapa wawili ambao walioshindana sana. Kila mmoja alijitahidi kuwataka wafuasi wampinge mwenzake na kutoa laana kubwa kwa mwenzake, na kuahidi zawadi kubwa za mbinguni kwa wasaidizi wake. Walishindana wao kwa wao siku nyingi. Kwa hiyo kwa muda Wyclife alipata kustarehe kidogo wakati walipokuwa kipingana wao kwa wao.TU 33.2

  Mafarakano hayo pamoja na uovu wote ulioletwa nayo yalitayarisha njia kwa matengenezo ya kanisa, maana watu waliona wazi maongozi ya upapa jinsi yalivyokuwa. Wyclife aliawaambia watu wafikiri na kuona kama mapapa mawili hao na mashindano yao si hakika kwamba wao ni wapinga Kristo!TU 33.3

  Wycliffe akikusudia kueneza nuru ya Injili kote katika nchi, alianzisha makundi ya wahubiri, ambao ni watu waongofu wa kweli waliokuwa tayari kueneza ukweli, Watu hawa walihubiri sokoni, katika njia kuu za mjini, waliwafikia wazee na wago-njwa, na maskini wakawasomea habari njema za neema ya Mungu.TU 33.4

  Katika chuo cha Oxford Wycliffe alihubiri neno la Mungu katika ukumbi wa chuo. Alitunukiwa heshima ya kuitwa Daktari wa Injili (Gospel Doctor). Lakini kazi kubwa aliyoifanya maishani mwake ni ile ya kutafsiri Biblia katika lugha ya Kiingereza ili kila mtu wa Uingereza aweza kusoma maajabu ya Mungu katika lugha yake.TU 33.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents