Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Alishikwa na Ugonjwa wa Hatari.

  Kazi ya Wyclife ilisimama kwa ghafla. Ingawa alikuwa hajafikia umri wa miaka sitini, kazi ngumu aliyoifanya, na shughuli za kujifunza, pamoja na mashambulio ya adui zake vilimdhoofisha sana na kuchakaza afya yake. Mara akashikwa na ugonjwa wa hatari sana. Watawa walidhani kuwa ataungama maovu aliyotenda kwa kupinga msimamo wa kanisa. Kwa hiyo walikwenda chumbani mwake wakitazamia kusikia maungamo yake. Wakamwambia, “Una mauti kinywani mwako. Jutia maovu yako, ukane mbele yetu maneno yote uliyotushutumia”TU 33.6

  Wycliffe aliyasikiliza maneno yao hali amenyamaza kimya. Kisha akawaomba wamwinue juu ya kitanda. Halafu akiwakazia macho, alisema kwa ujasiri, kwa sauti kuu iliyokuwa ikiwatetemesha mara nyingi, “Sitakufa, bali nitaishi na nitaendelea kushutumu maovu ya watawa” kwa fadhaha na aibu, watawa hao walitoka kwa haraka chumbani humo.TU 33.7

  Wycliffe aliishi na kuweka mikononi mwa watu wa nchi yake silaha kuu ya kuwapigia Warumi, yaani Biblia ambayo ilipangwa na mbingu ili iwaweke huru watu na kuwaangazia na kuwahubiria. Wycliffe alifahamu kuwa imebaki miaka michache ya kufanya kazi hiyo; aliona mapingano yaliyomkabili, lakini akifarijiwa na ahadi za neno la Mungu aliendelea mbele bila kusita. Akiwa na juhudi na moyo wa utendaji, na ujuzi mwingi, alikuwa ameandaliwa na Mungu kwa kazi hii kuu. Wycliffe akiwa kasisi wa Lutterworth, bila kujali dhoruba iliyokuwa ikivuma alijitia kazini mwake kamili.TU 34.1

  Mwishowe kazi ilikamilika yaani Biblia ya Kiingereza iliyotafsiriwa ikatokea. Mtengenezaji wa kanisa amefaulu kuwapatia watu wa Uingereza nuru ya neno la Mungu katika lugha yao, ambayo haitazimika kamwe. Ametenda makuu kwa kuvunja ngome ya ujinga na kuwapatia watu uhuru kamili na kuiangazia nuru nchi yake, kuliko shujaa apiganaye vita.TU 34.2

  Biblia ilipatikana tu kwa njia ya shida na kazi ngumu. Watu walipenda mno kupata Biblia, hata ikawa hazitoshelezi haja ya watu. Matajiri walinunua Biblia nzima na wengine walipata sehemu ya Biblia. Mara nyingi watu wa familia fulani fulani walishirikiana kununua Biblia moja nzima. Hivyo Biblia ya Wycliffe ilipata njia ya kuingia katika nyumba za watu.TU 34.3

  Sasa Wycliffe akafundisha mafundisho ya Kiprotestanti, tofauti na yale ya Kirumi yaana wokovu hupatikana kwa njia ya imani na kwamba Biblia ni kamili hasa haina kasoro. Imani hii mpya ilikubaliwa na kupokelewa na karibu nusu ya watu wa Uingereza.TU 34.4

  Kuonekana kwa maandiko kulifadhaisha utawala wa kanisa. Kwa wakati huo haikuwako sheria ya kupiga marufuku Biblia huko Uingereza, maana Biblia ilikuwa haijatafsiriwa katika lugha ya watu. Sheria hiyo iliwekwa baadaye na kusistizwa sana.TU 34.5

  Tena waongozi wa papa walifanya njama ya kunyamazisha huyu mtengenezaji wa Kanisa. Kwanza mkutano wa viongozi wa Rumi waliamua kuyaharamisha maandiko ya Wycliffe, yaani kuwa itakuwa ni maandiko haramu. Walipomshawishi mfalme kijana Richard II akakubaliana nao hivyo amri ya kifalme ikatangazwa kuwa mtu ye yote ambaye angeendelea kutoa mambo hayo yaliyopigwa marufuku angetiwa gerezani.TU 34.6

  Wycliffe akaomba rufaa kutoka kwa waongozi mpaka kwenye Bunge. Bila hofu aliwashitaki maaskofu mbele ya Bunge la taifa, na akadai matengenezo yafanywe ili kanisa lisitiwe madoa namna hii. Adui zake waliduwaa. Ilitazamiwa kuwa Wycliffe katika uzee wake, akiwa mwenyewe bila rafiki, atashindwa. Lakini badala yake, bunge likisisimka kwa habari za Wycliffe, likayafuta mashitaka yote yaliyotupwa juu ya mtengenezaji wa kanisa. Kwa hiyo Wycliffe aliwekwa huru tena.TU 34.7

  Mara ya tatu Wycliffe aliletwa hukumuni tena. Safari hii katika baraza kuu katika ufalme. Hapo kazi ya Wycliffe ingekomeshwa; ndivyo mapapa walivyodhani. Kama wangekamilisha makusudi yao, Wycliffe angetoka barazani kwenda motoni.TU 35.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents