Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  6/Mashujaa Wawili Wakabili Mauti

  Mapema katika karne ya tisa Biblia ilikuwa imetafsiriwa na kutawanywa kwa watu wa Bohemia. Ibada ya hadhara ilikuwa ikifanyika kwa lugha ya Wabohemia. Gregory VII alikusudia kuwatia watu utumwani. “Basi tangazo lilipotolewa la kupiga marufuku ibada ya hadhara katika lugha ya Bohemia ilifanyika katila lugha isiyojulikana” Lakini mbingu imeandaa watunzaji wa kweli yake, yaani kanisa. Watu wengi wa Waldenses na Albigenses walifukuzwa na mateso wakakimbilia Bohemia. Walifanya kazi sirisiri, kwa bidii. Kwa hiyo imani ya kweli ilihifadhiwa hapo.TU 39.1

  Kabla Huss hajatokea walikuwapo watu huko Bohemia walioyalaani maovu yaliyokuwa kanisani. Hofu ya maaskofu iliamshwa na mateso yakatokea juu ya injili. Baada ya muda amri ilitolewa kwamba watu wanaoabudu kinyume cha maongozi ya Rumi, lazima wachomwe moto. Lakini wakristo walitazama kufaulu kwa imani yao. Mmoja alipokuwa akichomwa alisema, “Atatokea mmoja katika watu, bila silaha wala cheo, wala hawatamshinda” Mmoja alikuwa anatokea tayari, ambaye ushuhuda wake juu ya Rumi, utayataharukisha mataifa.TU 39.2

  John Huss alizaliwa katika jamaa ya kawaida tu, na alifiwa na Baba yake mapema sana, akakua katika hali ya yatima. Mama yake ambaye ni mcha Mungu, aliyeyathamini mafundisho sana, aliazimu kuyapitisha kwa mwanawe. Huss alisomea katika shule za kawaida za kwao halafu akaingia katika chuko kikuu cha Prague, akipokewa kama mtoto yatima.TU 39.3

  Katika chuo kikuu Huss alisonga mbele kimaendeleo. hali yake ya upole ilimpatia heshima pote. Alikuwa mfuasi mwenye juhudi wa kanisa la Rumi. Alijitahidi kuzingatia mafundisho yote yaliyotelewa nao. Alipohitimu mafundisho ya Chuo kikuu aliingia kazi ya ukasisi. Alivyopanda upesi na kupata cheo aliungana na baraza la mfalme. Alifanywa kuwa mwalimu mtaalamu, baadaye akawa mkuu wa Chuo Kikuu. Mtoto yatima aliyeingia chuoni kwa rehema, amekuwa mkuu katika nchi yake na jina lake likajulikana katika Ulaya yote.TU 39.4

  Jerome, ambaye baadaye alikuwa mshiriki wa Huss, alileta maandiko ya Wycliffe kutoka Uingereza. Malkia wa Uingereza, ambaye aliongolewa na mahubiri ya Wycliffe alikuwa binti wa Bohemia. Kwa njia ya mvuto wake, kazi ya matengenezo ya kanisa ilienea katika nchi yake. Huss alielekea kuipenda kazi ya matengenezo ya kanisa. Alikuwa ameingia tayari katika barabara ambayo ingemwondoa kutoka Rumi, ingawa hakujua vizuri wakati huo.TU 40.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents