Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Picha mbili Zilimvutia Huss

  Wakati ule ule wageni wawili walitoka Uingereza wenye elimu, walikuwa wamepokea nuru ya Injili, nao wamekuja kuendeleza Prague. Haukupita muda mrefu, wakanyamazishwa, lakini kwa kuwa hawakutaka kuacha kusudi lao, wakatumia njia nyingine. Kwa kuwa walikuwa wachoraji wa picha pamoja na kuhubiri, wakachora picha mbili. Moja ilionyesha maingilio ya Yesu katika Yerusalemu, akiwa mpole, amepanda mwanapunda, (Mathayo 21:5) akifuatwa na wanafunzi wake wakiwa na mavazi ya vivi hivi na bila viatu. Picha nyingine ilikuwa na msafara wa Papa, akiwa na mavazi yake rasmi na taji yenye kung'aa akipanda farasi aliyepambwa vizuri, akitangulia na wenye matarumbeta, na kufuatwa na maaskofu katika mavazi yao rasmi.TU 40.2

  Watu wakakusanyika kuja kuangalia picha zao. Hakuna mtu ambaye alikosa kuzitambua. Kulikuwa na msukosuko mkubwa huko Prague, hata ikabidi wale wageni waondoke na kwenda zao. Lakini picha zile zilimwingia Huss moyoni sana, hata ikabidi asome sana maandiko ya Wycliffe na kuyatafakari.TU 40.3

  Ingawa alikuwa bado hajakubali mafundisho yote ya Wycliffe aliona tabia halisi ya papa, naye akalaani majivuno, kutakabari, na upotovu wa upapa.TU 40.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents