Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Prague Iliwekwa Chini ya Karantini

  Habari zilifika Rumi, na Huss akaitwa mbele ya papa. Kama akienda matokeo ni kifo tu. Mfalme na malkia wa Bohemia jamii ya Chuo Kikuu, watu mashuhuri wa wakuu wa serikali wote wakaungana kumsihi papa amwache Huss akae Prague asiende Rumi ili ajibu kwa kutuma mjumbe. Badala yake papa alitoa hukumu ya Huss na akautangazia mji wa Prague kuwa umewekwa chini ya karantini.TU 40.5

  Hukumu ya papa katikaTU 41.1

  kipindi hicho iliwashtua watu. Watu walimhesabu papa kuwa mwakilishi wa Mungu, kwamba yeye anazo funguo za mbinguni na za kuzimuni pia na waliamini kuwa papa asipopendezwa, hawezi kumtoa mtu aliyekufa kutoka ahera na kuingia raha ya milele. Huduma zote za kidini zilikomeshwa. Makanisa yalifunga. Ndoa zilifungiwa katika uwanja wa kanisa. Wafu walizikwa bila kufanyiwa ibada, na wakazikwa popote mahandakini au mbugani.TU 41.2

  Prague ilijaa ghasia nyingi. Watu walimlamu Huss, wakasema kuwa atolewe aende Rumi. Ili kutuliza ghasia, Huss aliondoka akaenda kwao kijijini. Lakini hakukoma kufanya kazi yake, ila alisafiri safari akiwahubiria watu waliopendezwa. Ghasia zilipopungua huko Prague Huss alirudi huko kulihubiri neno la Mungu. Maadui zake walikuwa hodari lakini Malkia pamoja na watu wengine mashuhuri walikuwa rafiki zake, na watu wengi pia walikuwa upande wake.TU 41.3

  Huss alisimama mwenyewe katika kazi. Halafu Jerome aliungana naye. Watu hawa wawili waliungana kikamilifu hata mauti haikuwatenga. Sifa bora ndizo zilizofanya tabia zao zifae, Huss alikuwa nazo zaidi. Jerome ambaye alikuwa mnyenyekevu alikubaliana na Huss kamili. Wote kwa pamoja wakaieneza kazi ya matengenezo ya kanisa na kuisukuma mbele.TU 41.4

  Mungu aliwajalia watu hawa kupata nuru, na kuwaonyesha makosa mengi ya kanisa la Rumi. Walakini hawakupata nuru yoyote iliyotakiwa kutolewa kwa ulimwengu. Mungu alikuwa akiwaongoza watu polepole kutoka katika giza la Rumi, hatua kwa hatua maana wasingeweza kupata yote mara moja na kuyachukua. Ni sawa na mwanga wa jua kwa wote walio gizani, huwazukia kidogo kidogo, ama kama nuru ingewazukia yote ingewapoteza. Kwa hiyo Mungu aliwafunulia taratibu.TU 41.5

  Farakano kanisani liliendelea. Sasa mapapa watatu walikuwa wakishindania ukubwa. Mashindano yao yalileta fujo nyingi katika ukristo. Hawakutosheka na kulaumiana peke yake, lakini kila mmoja alitafuta silaha na askari. Bila shaka fedha zilikuwa lazima zipatikane. Kwa hiyo zawadi, vyeo na mibaraka ya kanisa vikatolewa kwa kuuzwa.TU 41.6

  Kwa ujasiri Huss akaunguruma kuhusu machafuko hayo ambayo ni machukizo yanayoleta aibu kwa dini. Akashambulia kwa ushujaa kabisa. Watu wakailaumu Rumi wazi kuwa inaaibisha dini.TU 41.7

  Mara tena Praggue ikaonekana kuwa kwenye ukingo wa kumwaga damu kwa mapambano. Kama ilivyokuwa zamani mtumishi wa Mungu alivyolaumiwa kuwa “Mtaabisha Israeli” 1 Fal. 18:17. Mji ukawekwa tena chini ya karantini na Huss akaondoka kwenda kwao kijijini. Ilimpasa aseme kwa nguvu zaidi kuhusu ukristo kabla hajauawa kama mashahidi wa kweli.TU 41.8

  Baraza kuu liliitishwa kukutana huko Constance (Kusini Magharibi ya Ujerumani). Liliitishwa kwa matakwa ya mfalme Sigismud, kwa ajili ya mmoja wa wale mapapa watatu, aitwaye John XXIII. Papa John, mwenye tabia ya vivi hivi, ndiye alishika kazi ya uchunguzi. Naye hakuweza kupinga matakwa ya mfalme Sigismund. Kusudi la baraza hili lilikuwa ni kutafuta njia ya kumaliza farakano lililomo kanisani; na kung'olea mbali mizizi ya uzushi. Wale mapapa wawili aliokuwa wanashindana walitakiwa wafike barazani pamoja na John Huss. Wale mapapa waliwakilishwa na wajumbe. Papa John alikuwa na wasiwasi sana, akiogopa asije akatakiwa kueleza sababu za kuhafifisha umaarufu wa taji yao na heshima yao. Walakini aliingia katika mji wa Constance kwa fahari na kishindo akifuatana na makasisi, na wafuasi wa mfalme. Juu ya kichwa chake alikuwa na chombo cha dhahabu kikishikiliwa na mahakimu wanne. Mkate wa kufanyia ibada ya pasaka ulikuwa umechukuliwa mbele yake na mavazi ya maaskofu na wakuu wote, yalikamilisha onekano la fahari kuu.TU 42.1

  Wakati huo huo msafiri mwingine pia alikuwa akija Constance. Huss aliagana na rafiki zake akienda Constance kana kwamba hawataonana kamwe. Alisafiri safari ambayo alijisikia kana kwamba anakwenda kuchomwa moto kwenye mti. Alipata mlinzi kutoka kwa mfalme wa Bohemia na mwingine toka kwa Mfalme Sixmund. Lakini alijitayarisha kwa kifo.TU 42.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents