Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mlinzi Toka kwa Mfalme

  Katika barua aliyowaandikia rafiki zake alisema, “Ndugu, zangu ninaondoka nikiwa na mlinzi toka kwa mfalme ili nikakutane na maadui wengi wenye kufisha. Yesu aliteseka kwa ajili ya wapenzi wake; je, sisi tutaona ajabu kufuata kielelezo chake?….. Kwa hiyo wapendwa, ikiwa kifo changu kitamtukuza, ombeni basi ili kije upesi, na kwamba aniwezeshe kusimama kiume katika matatizo yote…. Hebu na tuombe kwa Mungu... kwamba nisivunje hata neno moja la heshim ya Injili, ili niwaachie ndugu zangu kielelezo safi cha kufuata”.TU 42.3

  Katika barua nyingine, Huss alisema kwa unyenyekevu makosa aliyofanya ya kufurahia kuvaa mavazi ya fahari na muda liopoteza kwa kufanya mambo hafifu. Akaongeza, Hebu utukufu wa Mungu, na wokovu wa watu vijaze mawazo yenu, wala siyo mali na mashamba. Jihadharini na kupamba nyumba zenu kuliko kupamba mioyo yenu na zaidi ya yote kazaneni na mambo ya kiroho. Mwe wacha Mungu na wanyenyekevu, mkichukuliana na maskini. Msimalize mali zenu kwa ulafi.TU 43.1

  Huko Constance Hus alipewa uhuru kamili. Pamoja na mlinzi wa mfalme, papa pia alimwongezea ulinzi zaidi. Lakini pamoja na hayo yote amri ilitoka kwa Papa kwamba Huss akamatwe na kutiwa kifungoni. Baadaye alihamishwa na kufungiwa ngomeni ng'ambo ya mto Rhine, na huko akawa mfungwa hasa. Halafu papa naye alitiwa kifungoni katika ngome ile ile alimokuwa Huss. Alipatikana na hatia ya ufedhuli, uuaji, biashara haramu ya uasherati. Dhambi ambazo hazifai kutajwa kwa mtu kama yeye. Baadaye alinyang'anywa kofia yake ya heshima. Hata wale mapapa waliokuwa wakishindania ukubwa waliondolewa pia, akachaguliwa papa mwingine.TU 43.2

  Ingawa papa mwenyewe amepatikana na dhambi kubwa kuliko Huss kama alivyoshitakiwa na mapadri, hata hivyo baraza lile lile lililowashusha mapapa kwa ajili ya ukorofi wao, liliendelea kumwangamiza Huss, mtengenezaji wa kanisa. Kufungwa kwa Huss kuliamsha uchungu mwingi katika nchi ya Bohemia. Mfalme akakataa kwa ujeuri kwamba Huss asishitakiwe. Lakini maadui wa Huss wakaleta mashitaka kwamba, yeye hana imani bali ni mzushi. Wakaendela kushindilia mambo kwake, ingawa alikuwa na ulinzi toka kwa wafalme.TU 43.3

  Huss akiteseka kifungoni, mahali penye unyevu, alipata ugonjwa uliomdhoofisha sana. Walakini hata hivyo aliletwa mahakamani kujibu mashitaka. Alisimama mbele ya mfalme akiwa na pingu mikononi na miguuni. Mfalme alikuwa na huruma kwake tangu hapo. Huss alitetea ukweli na kuyataja maovu ya maaskofu wa Rumi Dhahiri. Alipoulizwa kuchagua kati ya kukana imani yake na kuchomwa moto akifungwa mtini, alichagua kufa kuliko kukana ukweli wa imani yake.TU 43.4

  Neema ya Mungu ilimsaidia. Wakati alipokuwa anangoja mwisho wake, alikuwa mtulivu na amani ya Mungu ilimjaza. Alisema, “Ninaandika barua hii nikiwa gerezani mkono wangu ukiwa na pingu, huku nikingojea utekelezaji wa hukumu juu yangu kesho…. Wakati tutakapokutana kwa neema ya Mungu huko paradiso, katika maisha ya baadaye, utaelewa jinsi Mungu mwenye rehema alivyojidhihirisha kwangu, jinsi alivyonisaidia, katika majaribu na katika dhiki.”TU 44.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents