Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ushindi Unaonekana Kwa Njozi

  Katika kifungo chake aliona ushindi wa imani ya kweli kimawazo. Katika ndoto alimwona papa na maaskofu wakiondoa picha ya Kristo ambayo aliyoichora kwenye ukuta huko Prague. Ndoto hiyo ilimwudhi, lakini kesho yake aliona ndoto nyingine yenye picha zaidi ya hiyo iliyofutwa. Aliona picha nyingi, tena zenye kung'aa zaidi zimechorwa kila mahali... Wachoraji... wakiwa wamezungukwa na kundi kubwa la watu wakisema, “Sasa Papa na maaskofu wake na waje waone, hawawezi kuzifuta tena” Mtengenezaji wa kanisa alisema, “Sura ya Kristo haiwezi kufutika kamwe. Wametaka kuiharibu, lakini itachorwa upya mioyoni mwa watu na wahubiri wa Injili vizuri zaidi kuliko mimi”TU 44.2

  Mara ya mwisho, Huss aliletwa mahakamani, ambapo palikuwa pamejaa na penye fahari kuu. Palikuwako mfalme, wana wa kifalme, wajumbe, wakuu wa Roma, maaksofu, makasisi na kundi kubwa la watu.TU 44.3

  Huss akitakiwa mara ya pili kutoa uamuzi wake: Kukana imani, au kufa, Huss alikanusha kwa nguvu kwamba msimamo wake ni ule ule na kushikilia imani yake. Akimkazia mfalme macho, alisema “Ninaazimu kusimama katika mahakama hii kwa nia yangu mwenyewe, nikiwa na haki ya kupata ulinzi wa taifa, na nikiwa na imani ya mfalme ambaye nasimama mbele yake.” Mfalme Sigismund akabadilika uso, kadri macho ya watu wote walipomtazama.TU 44.4

  Baada ya kutamka maneno hayo, hali ya fedheha ilianza. Akisihiwa tena kukana imani, Huss alijibu huku akiwaelekea watu: “Niutazame uso gani? Sio wa mbinguni? Nawezaje kutazama watu ambao niliwahubiri Injili ya kweli? La, nauhesabu wokovu wao kuwa una thamani zaidi ya mwili wangu huu wa kimaskini, ambao umetajwa kwamba ufe” Mavazi ya kikuhani yalianza kuvuliwa moja moja wakati maaskofu wakijitayarisha kumwua huku wakimlaani. Mwisho wakamvalisha kofia ya karatasi ya kiaskofu ambayo ilikuwa imechorwa sanamu za mashetani, maneno yaliyoandikwa kwamba: “Mzushi mkuu” kwa upande. Huss akasema “Furaha kuu”. Yesu, ninavaa taji hii ya aibu kwa ajili yako, ambapo wewe ulivaa taji ya miiba kwa ajili yangu.TU 44.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents