Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Huss Achomwa Moto Mtini.

  Sasa aliongozwa kwenda nje, Kundi kuu la watu lilimfuata. Matayarisho yote ya kuwasha moto yalikamilika, Huss alisihiwa tena ili aungame makosa ili ajiokoe. Akasema, “Nikane nini? Kuna kosa gani? Mimi sijui kosa lolote nililofanya”. “Namwita Mungu awe shahidi kwamba mambo yote niliyohubiri na kuyaandika, yalihusu wokovu wa watu, ili waepukane na dhambi na wasipotee milele. Kwa hiyo ninayo furaha kuu kwa kuuthibitisha ukwelli huo nilioandika na kuhubiri kwa damu yangu mwenyewe”.TU 45.1

  Moto ulipowashwa katika mti alikofungiwa, alianza kuimba. “Yesu mwana wa Daudi unihurumie”. Aliendelea kuimba hivyo mpaka sauti yake ikaoma kwa milele, alipomalizikia katika ndimi za moto. Mfuasi wa Papa akizungumza baadaye, kuhusu kifo cha Huss na Jerome ambaye alichomwa moto baada ya Huss, akasema “Huss na Jerome walijitayarisha kwa kufa, kama wanavyojitayarisha kwa arusi. Hawakutoa neno la kulalamika kwa ajili ya maumivu. Moto ulipowashwa wao walianza kuimba. Wala ukali wa moto haukuweza kuzima sauti zao mpaka walipomalizikia humo. Mwili wa Huss ulipokwisha kutetekea majivu yake yalikusanywa na kutupwa katika mto wa Rhine, katika nchi zote mfano wa mbegu inavyotawanyika. Katika nchi ambazo hazikujua ujumbe wa Injili kutatokea matunda mengi, ushuhuda wa Injili. Sauti ya Huss iliyosikika katika mahakama ya Constance ilitoa mwangwi utakaosikika katika vizazi vijavyo. Kielelezo chake kilitia moyo wa imara kwa watu maelefu ili wakikabiliwa na kifo wasiogope. Kifo chake kimethibitisha ulimwenguni ukatili wa Rumi. Maadui wa haki waliendeleza mbele kusudi lao la uharibifu!”TU 45.2

  Hata hivyo damu ya shahidi mwingine lazima ishuhudie ukweli. Jerome alikuwa amemtia Huss moyo wa uthabiti, akisema, kwamba ikiwa itamlazimu apate hatari yeye atamsaidia. Aliposikia kuwa Huss amefungwa, Jerome alijitayarisha kutimiza ahadi yake. Hivyo alianza safari ya kwenda Constance bila kuwa na ulinzi wowote. Alipofika alijua kwamba aliingia hatarini na hatamsaidia lolote Huss. Alitoroka, lakini alikamwatwa na kurudishwa kwa pingu. Alipofikishwa mahakamani mara ya kwanza, usemi wake ulikutana na makelele ya mkutano yakisema, “Motoni, Motoni” Kisha alitupwa kifungoni akilishwa chakula haba. Ukatili aliotendewa ulimletea ugonjwa, nusura ya kufa. Hapo adui zake walikuwa na wasiwasi kwamba kama angekufa kwa ugonjwa, wangekuwa wamepoteza tazamio lao la kumchoma motoni, hivyo walimtunza ili asife. Alikaa kifungoni kwa muda wa mwaka mzima.TU 45.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents