Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jerome Atubu na Kuwa na Ujasiri

  Baada ya muda mfupi Jerome alifikishwa tena mahakamani. Kule kukiri kwa kwanza alikokiri kwamba ameacha imani yake, na kuwa atashikamana na mafundisho ya Rumi hakukuwaridhisha mahakimu. Angejiokoa tu, kwa maungamo kamili kuwa hana uhusiano tena na mafundisho ya kweli. Lakini aliazimu kukanusa maneno yake kwamba ameacha imani yake. Alikusudia kudhihirisha imani yake wazi na kufuata nyayo za mwenzake aliyechomwa moto. Kwa hiyo akafanya hivyo.TU 46.3

  Akataka apewe muda wa kujitetea vizuri kama mtu anayekuwa tayari kufa. Maaskofu walisisitiza kwamba Jerome alilaumu ukatili unaotendwa, bila haki, Akasema “Mmenifunga siku mia tatu na arobaini katika gereza chafu sana, mkasikiliza tu mambo ya adui zangu, na ya kwangu mkakataa kuyasikiliza…… Msinitendee dhambi, mkaiacha haki. Kwangu mimi, si kitu, mimi ni mtu dhaifu tu, na maisha yangu hayana maana yoyote, na ninapowasihi msinihukumu kikatili, hujisemea maneno yangu tu sio yenu”TU 47.1

  Mwisho walikubali ombi lake. Jerome alipiga magoti mbele ya mahakimu, akaomba Roho wa Mungu ayaongoze mawazo yake, ili asiseme mapotofu. Kwake, siku hiyo ahadi ya Yesu ilitimia, kwamba: “Lakini hapo watakapowapeleka, msifikirifikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni roho wa Baba yenu aliye ndani yenu” Mathayo 10:19-20.TU 47.2

  Kwa muda wa mwaka mzima Jerome alikaa kifungoni, akiwa hawezi kuona wala kusoma. Hata hivyo alipozungumza wakati wa kujitetea, usemi wake ulikuwa wazi na wenye nguvu kama ulivyoandaliwa vema na mtu aliyekuwa na nafasi ya kujitayarisha. Alitaja orodha ndefu ya watu wema ambao walitendewa ukatili na mahakimu waovu. Katika karne zote, watu wanyofu walitafuta kuinua hali za watu walitupwa nje. Kristo mwenyewe alihukumiwa sawa na watenda maovu. Alihukumiwa na mahakimu wasio haki.TU 47.3

  Sasa Jerome aliungama makosa aliyofanya safari ya kwanza, aliposema kuwa anaikana imani yake. Sasa alitoa ushuhuda wake wazi na kwamba msimamo wake ni sawa na ule wa Huss, aliyeuawa, yaani mfia dini. Alisema, “Nilimfahamu Huss tangu utoto wake. Alikuwa mtu maarufu, mwenye haki, na mtakatifu. Alihukumiwa, walakini alikuwa mwenye haki …… Hata mimi niko tayari kufa. Sitayaepuka mateso yanayonikabili, ambayo yametayarishwa na adui zangu. Najua kuwa wao ni mashahidi wa uongo, ambao siku moja watatoa hesabu mbele za Mungu ya Matendo yao maovu, maana hakuna kitu asichojua”TU 47.4

  Jerome aliendelea kusema, “Dhambi zote nilizotenda tangu utoto wangu, hakuna hata moja inayonishitaki katika dhamira yangu, na kunijutisha, sawa na ile niliyofanya hapa wakati nilipowashutumu Wycliffe na Huss kuwa ni wazushi, hasa Huss ambaye ni bwana wangu na rafiki yangu. Ndiyo na ungama dhambi hiyo kwa moyo wangu wote, kwamba nilikosa kabisa niliposhuhudia kuwa mafundisho yao ni ya uongo, nikiogopa tu kufa. Kwa hiyo usemi huo naukanusha hasa. Mwenyenzi Mungu anisamehe, hasa dhambi hii.”TU 47.5

  Akiwasonda mahakimu, alisema kwa ushujaa: “Ninyi mliwahukumu Wycliffe na Huss …. Kwa mambo ambayo hakika yasiyokanika …. Hata mimi pia nafikiri kama wao”TU 48.1

  Hotuba yake iliingiliwa kati. Maaskofu wakiwa wamejaa ghadhabu nyingi, walipaza sauti na kusema “Tunahitaji ushahidi gani zaidi? Tumeona kwa macho yetu ukaidi wa mzushi huyu”.TU 48.2

  Jerome akisimama imara alisema: “Ninyi, mnadhani kuwa mimi niliogopa kufa? Mmenifunga gerezani mwaka mzima mahali pabaya kabisa, panazidi kifo. Siwezi kueleza hali ya namna hiyo inayotendwa kwa wakristo”TU 48.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents