Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Apangiwa Kufungwa na Kuuawa

  Lakini yeye alijibu: “Nionyesheni fungu la Maandiko kuthibitisha kosa langu, nami nitakubali. Mmoja wa washawishi wake alisema,” Maandiko matakatifu ndiyo yenye kuhukumu kitu? Nani atayafahamu yasipotafsiriwa na kanisa?TU 48.4

  Jerome akasema, Je, mapokeo ya wanadamu yanathaminiwa kuliko Injili ya Mwokozi? Akajibiwa kwa kishindo, “Mzushi!” Mmoja akasema “Nasikitika kuwa nimepoteza muda wangu bure kukusihi, naona kuwa Ibilisi anakusukuma na amekujaza”TU 48.5

  Kabla ya kupita muda mrefu aliongozwa kwenda mahali pale Huss alipochomewa. Alienda akiimba njia nzima. Uso wake uling'aa na alikuwa ametulia kabisa. Hofu ya mauti haikumtisha. Mwenye kuwasha moto alipokuwa tayari, Jerome alimwambia, “Anzia kuwasha upande wa uso wangu, usianzie nyuma, maana kama ningeogopa moto nisingekuwa hapa.”TU 48.6

  Maneno yake ya mwisho yalikuwa ni sala “Bwana mwenye uwezo, nihurumie. Unisamehe dhambi zangu maana unajua kuwa mimi nimependa kweli yako siku zote.” Baada ya kuteketea, majivu yake yalikusanywa na kutupwa katika mto wa Rhine, sawasawa na ya Huss. Ndivyo wajumbe wachukuzi wa nuru wa Mungu walivyopotea.TU 49.1

  Kifo cha Huss kilileta hasira na ghasia katika Bohemia. Taifa lote lilimtaja kuwa mwalimu mwaminifu, afundishaye kweli ya Injili. Mahakama ilishitakiwa kwa kosa la kuua. Mafundisho ya Huss yaliwavuta watu wengi kuliko hapo zamani. Na watu wengi waliamini. Basi papa na mfalme waliungana pamoja ili kuangamiza watu hawa wenye imani. Kwa hiyo majeshi ya mfalme Sigismund yalimwagwa Bohemia kwa kazi hiyo.TU 49.2

  Lakini mkombozi alitokea Ziska, ambaye alikuwa amiri jeshi hodari sana, aliongoza majeshi ya bohemia. Watu hao wakiutumainia msaada wa Mugu waliweza kuyakabili majeshi makuu yaliyowavamia. Mfalme alivamia Bohemia mara nyingi na kila mara majeshi yake yalirudishwa nyuma kwa hasara kubwa. Wafuasi wa Huss walistushwa na kifo cha ukatili, wakawa wakali, wala hakuna kitu kilichoweza kusimama mbele yao. Shujaa Ziska alikufa, na mahali pake pakashikwa na shujaa zaidi jina lake Procopius.TU 49.3

  Papa alitangaza vita na wafuasi wa Huss. Kwa hiyo jeshi kuu mno likapelekwa Bohemia kivamizi. Matokeo ni kuwa likashindwa vibaya kwa hasara kuu. Katika nchi zote za Ulaya mahali papa alipokuwa akitawala michango ilianzishwa ya fedha na mali, askari, zana za vita na kadhalika.TU 49.4

  Basi jeshi kubwa mno likavamia Bohemia. Watu wakaungana kuwafukuza. Majeshi mawili yakakabiliana ila tu mto uliwatenga. Wavamizi walikuwa wengi mno. Badala ya kuvuka mto na kuwashambulia wafuasi wa Huss, walisimama wakiwatazama wapiganaji.TU 49.5

  Kwa ghafla kishindo cha kimuujiza kikawaangukia wavamizi. Mara wakatawanyika kama wanafukuzwa na uwezo usiojulikana. Wafuasi wa Huss wakawakimbiza na kuwaangamiza wengi sana. Vita badala ya kuharibu Bohemia, ilistawisha.TU 49.6

  Baada ya miaka michache chini ya papa mwingine, jeshi likatumwa kuvamia Bohemia kwa mguu. Wafuasi wa Huss wakajifanya kukimbia ili wawavute adui waingie katikati ya nchi. Mwisho jeshi la Procopius likawashambulia. Hofu kuu iliwashika hata kabla Wahuss hawajafika. Watu wote wakuu, majemadari, askari wakakimbia huku wakitupa silaha zao chini. Mara hiyo tena wakaangukia mikononi mwa Wahuss.TU 50.1

  Mara nyingine tena jeshi lililofundishwa lilipotumwa likakimbizwa na uwezo wa kimuujiza. Aliyempigania Gideon na watu mia tatu, ndiye aliyewapigania wafuasi wa Huss. Zaburi. 7:19-25, Zaburi 53:5TU 50.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents