Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Walisalitiwa Kijanja

  Viongozi wa papa mwishowe walitumia njia ya mazungumzo ya kijanja kama kwamba wana nia njema kumbe sivyo. Makubaliano yalifikiwa ambayo yaliwasaliti watu wa Bohemia, na kuwaweka chini ya mamlala ya Papa yaani utawala wa Rumi. Watu wa Bohemia walitaja masharti manne ya amani baina yao na Rumi (1) Uhuru wa kuhubiri na kufundisha Biblia bila kuingiliwa; (2) Haki ya kanisa zima kutumia mkate na divai wakati wa Meza ya Bwana, na uhuru wa kuabudu kwa kutumia lugha ya watu. (3) Waongozi wa kanisa (maaskofu, mapadri, makasisi na kadhalika) kutojihusisha na mambo ya serikali, wala kuchaguliwa kwenye madaraka serikalini. (4)Kuhusu uvunjaji wa sheria, mahakama za serikali ziwashughulikie wote, wanaohusika, kama ni askofu au mkristo wa kawaida. Utawala wa papa ulikubali mambo hayo manne, ila tu haki ya kuyaeleza na kuyafafanua iwe juu ya baraza ambalo huendeshwa na papa na mfalme. Rumi ikafanikiwa kwa njia ya udanganyifu na hila ambayo ilishindwa kwa njia ya kutumia nguvu. Katika kusafiri na kufafanua masharti ya watu wa Huss, papa alitumia ujanja wa kuyapotosha, na kuonekana kwamba yanatokana na Biblia. Hivyo alifaulu kwa hila kuendeleza upotofu wake.TU 50.3

  Watu wengi wa Bohemia walipoona kuwa wamesalitiwa hawakukubali kushikana na mapatano hayo. Ugomvi ukazuka baina yao. Procopius alikufa. Na uhuru wa Bohemia ukaangamia.TU 50.4

  Mara nyingine tena majeshi ya kigeni yalivamia Bohemia na wale waliokuwa waaminifu kwa Injili walikabiliwa na mateso ya umwagaji damu. Hata hivyo walisimama kishujaa. Ingawa iliwalazimu kukimbia mapangoni walidumu kusoma neno la Mungu na kuabudu. Kwa njia ya wajumbe watumwa kwa siri kwenda nchi yingine, walielewa kuwa katika milima ya Alps kulikuwepo na kanisa la watu waaminifu wacha Mungu wanaoshika kanuni ya Biblia na kuupinga upotofu wa rumi. Basi wakawa wakiwasiliana na Waldeses kwa furaha, maana ni wenzao katika ukristo.TU 51.1

  Watu wa Bohemia wakishikilia kanuni za Biblia walisimama imara wakingoja na hata katika nyakati za giza la mateso makali walizidi kuwa imara kama walinzi wa usiku wangojavyo mapambazuko ya asubuhi.TU 51.2

  Marejeo: TU 51.3

  Wylie, bk 3, ch. 1 ibid TU 51.4

  Bonnechose, Vol. 1 pp. 147, 148. TU 51.5

  Ibid., pp. 148-149 TU 51.6

  Ibidi pp. 247 TU 51.7

  Jacques lenfant. History of Concil of Constance Vol. 1 p. 516 TU 51.8

  Bonnechose. Vol. 2p. 84 TU 51.9

  D'Aubigne, bk.1.ch. 6 TU 51.10

  Bonnechose, Vol. 2 p. 84 TU 51.11

  Wylie, bk. 3 ch.7 TU 51.12

  Ibid. TU 51.13

  Ibid. TU 51.14

  Bonnechose,, Vol. 1, p.234 TU 51.15

  Ibid. Vol 2 p. 141 TU 51.16

  Ibid. p. 146 — 147 TU 51.17

  Bonnechose, vol.2, p. 168 TU 51.18

  Wylie, bk. 3, ch. 10 TU 51.19

  Bonnechose, Vol. 2, p. 168. TU 51.20

  Wylie, bk. 3, ch. 17 TU 51.21

  Ibid. ch. 18 TU 51.22

  Ibid. ch.19TU 51.23

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents