Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  7\ Luther, Shujaa Kwa Wakati Wake

  Katika watu waliotumiwa na Mungu kulitoa kanisa katika giza la upapa, na kuwaleta katika nuru ya kweli ya Biblia na imani halisi, Martin Luther ni mmoja wa hao katika mstari wa mbele. Hakujua kuogopa kitu kingine ila Mungu tu, wala hakujua msingi mwingine wa imani, ila ule uliomo katika Biblia. Alikuwa shujaa kwa wakati wake.TU 52.1

  Alikulia katika jamaa ya mkulima katika nchi ya Ujerumani. Baba yake alikusudia kuwa afanye kazi ya uanasheria, lakini Mungu alimkusudia awe mjenzi wa hekalu lake ambalo lilikuwa likikua pole pole kwa karne nyingi. Shule ya Mungu iliyomfundisha Luther mpaka akahitimu ilikuwa shida, dhiki na maisha magumu sana.TU 52.2

  Baba yake Luther alikuwa mtu hodari, mwenye nia thabiti. Mawazo yake yalimwamisha kuwa maisha ya utawa na kawaida zake, hayafai. Alichukizwa Luther alipoingia katika hali ya utawa bila kumwuliza. Ilipita miaka miwili kabla baba yake Luther hajapatanishwa na mwanawe, hata hivyo nia yake ilikuwa ile ile.TU 52.3

  Wazazi wa Luther walijitahidi kuwaelimisha watoto katika neno la Mungu. Juhudi yao ilikuwa ya kuendelea kuwatayarisha watoto wao wafae kutumika maishani, wakati mwingine walikazana kwa uaminifu hata Luther mwenyewe alipendezwa pia na nia hiyo.TU 52.4

  Katika shule, Luther alitendewa kikatili. Mara nyingi alishinda na njaa. Hali ya mawazo ya kidini ilimwogofya. Alipolala usiku alikuwa na moyo wa huzuni. Mara nyingi alimdhania Mungu kuwa ni jitu kali lisilo na huruma, kwa wakosaji, kuliko Baba wa mbinguni mwenye huruma.TU 52.5

  Alipoingia katika chuo kikuu cha Erfurt, alikuwa na hali nzuri kuliko kwanza. Wazazi wake wakiwa wamejiwekea akiba kidogo, waliweza kumsaidia katika mahitaji yake, na marafiki zake wema waliweza kumfariji ajione nafuu. Kwa njia hiyo hapa mawazo yake alipanuka. Kwa bidii yake mwisho akajikuta juu kati ya wenzake.TU 52.6

  Luter hakuacha kuomba kila siku. Roho yake ilikuwa na faraja na maongozi ya juu. Kila mara alisema “Kuomba vema ni bora, ni nusu ya mafundisho”TU 52.7

  Siku moja aligundua Biblia ya Kilatini katika maktaba ya Chuo Kikuu. Alikuwa hajaona kitabu hicho. Alikuwa amesikia sehemu ya Injili na nyaraka, ambazo alidhani kuwa ndizo Biblia kamili. Sasa kwa mara ya kwanza katika maisha yake, alisoma neno kamili la Mungu. Sasa kwa mara ya kwanza katika maisha yake, alisoma neno kamili la Mungu. Alisoma kwa kicho na mshangao mkubwa, huku akitulia mara ya kwanza na kusema, “Lo Mungu anijalie nipate Biblia yangu mwenyewe!” Malaika walikuwa karibu naye. Miali ya nuru ya neno la Mungu ilifunua hazina kuu katika mawazo yake. Akajiona wazi kuwa yu mwenye dhambi.TU 53.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents