Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Amani na Mungu

  Akitamani kuwa na amani pamoja na Mungu, Luther alijitahidi kuishi katika hali ya utawa. Katika hali hiyo alitakiwa kufanya kazi ngumu sana, yaani kutumika kitumwa, na kuomba omba vitu nyumba kwa nyumba. Alivumilia mambo hayo yote akidhani kuwa hivyo ndiyo njia ya kusamehewa dhambi zake.TU 53.2

  Akitumika kwa jinsi hiyo, na kujinyima usingizi saa za kulala, na hata saa za kula pia. Luther alipendelea kusoma biblia kila alipopata nafasi hata kama ni kidogo. Alipata Biblia imefungwa ukutani kwa mnyororo, katika nyumba ya watawa, kwa hiyo alienda kuko kila mara ili kuisoma.TU 53.3

  Aliishi maisha ya kitawa kweli kweli. Alifunga kila mara, na kukesha usiku kucha. Alijiadhibu mwenyewe ili kufukuza dhambi zilizomo ndani yake. Baadaye alisema, “Kama watawa wataingia mbinguni kwa njia ya kuishi kitawa, mimi bila shaka nitaingia…. Ikiwa inatakiwa zaidi ya haya, mimi nitaendelea hata kufa!” Pamoja na juhudi hizo zote, lakini Luther hakupata pumziko, wala faraja yoyote. Mwisho alifika ukingoni mwa kukata tamaa.TU 53.4

  Ilipoonekana kwamba mambo yote yamekuwa kazi bure. Mungu alimwinulia mwenzi jina Staupitz. Huyu Staupitz, alimfunulia Luther neno la Mungu, mawazo yake yakafunguka.TU 53.5

  Staupitz, alimshauri kumtazama Yesu, wala asijitumainie mwenyewe. Akamwambia “Badala ya kujitesa ili usamehewe dhambi, jikabidhi katika mikono ya Mwokozi. Mtumainie yeye na haki yake tu, ukitumainia dhabihu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Maana alikufa ili tuishi…. Mwana wa Mungu…. Alifanyika kuwa mwanadamu ili kukupatia uhakika wa rehema za Mungu. …Mpende yeye, maana yeye alikuwepo kwanza.” Maneno ya Staupitz yaliugusa moyo wa Luther, akapata faraja katika moyo wake wenye wasiwasi.TU 53.6

  Luther alipofanywa kuwa kasisi, aliitwa kuwa mwalimu katika chuo kikuu cha Wittnemberg. Alianza kufundisha juu ya Zaburi na Injili na Nyaraka kwa makundi ya watu waliokuwa na hamu sana kusikia. Staupitz akamshauri apande mimbarani ili ahubiri. Lakini Luther alijiona kuwa hastahili kuhubiri badala ya Kristo. Baada ya mashindano makubwa ndipo alikubali mashauri ya rafiki yake, yaani ahubiri. Alikuwa mtu hodari katika maandiko na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Maelezo yake ya wazi na ujuzi wake wa maandiko, viliwavutia watu katika kuzibua mioyo yao.TU 54.1

  Wakati huo Luther akiwa bado mwana wa kweli wa Rumi, hakudhani kuwa atakuwa mwingine. Alipotakiwa kwenda kuzuru Rumi, alisafiri kwa miguu, akilala katika nyumba za watawa njiani. Alishangazwa fahari aliyoona. Watawa walikuwa wakiishi katika nyumba za fahari kabisa wakivaa mavazi rasmi yenye bei ghali sana, na kula chakula cha kianasa kweli kweli. Mawazo ya Luther yakatatanika.TU 54.2

  Baadaye, kwa mbali aliuona mji wa Rumi ukijengwa kwenye vilima saba. Akajitandaza chini akisema “Rumi mtakatifu Nakusalimu!” alizuru makanisa, akisikiliza hadithi za ajabu za mapadri na watawa na kushiriki katika kawaida zote zilizotakiwa. Kila mahali aliona mambo ya ajabu. Maovu yaliyoonekana kati ya viongozi, ufedhuli wa maaskofu vyote vilimstaajabisha. Alishangazwa na upotovu uliotendwa hata wakati wa huduma. Alikuta matendo ya uasherati ulevi na uchafu wa kila namna. Aliandika akisema hatuwezi kuwaza kwamba dhambi mbaya hizi hutendeka Rumi. Watu husema “Kama iko jehanam, Rumi imejengwa juu yake!”TU 54.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents