Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ukweli Juu ya Ngazi ya Pilato.

  Msamaha umeahidiwa na papa kwa mtu yeyote atakayepanda ngazi ya Pilato kwa magoti. Yasemekana ngazi hiyo ililetwa kwa muujiza Rumi toka Yerusalemu. Siku moja Luther alikuwa akizipanda ngazi hizo, wakati aliposikia sauti kama ngurumo ikisema “Mwenye haki ataishi kwa Imani” Warumi 1:17. Mara akasimama kwa hofu na mshangao. Tokea siku hiyo aliona dhahiri jinsi ilivyo upuuzi wa kutegemea matendo mema, kwa wokovu. Akageuzia Rumi uso wake, yaani akaondoa matumaini yake kwa Rumi. Tokea wakati huo nia ya mtengano wa Rumi ikazidi kukua mpaka akavunja uhusiano wote na kanisa la mapapa.TU 54.4

  Baada ya kurudi kutoka Rumi Luther alipokea shahada ya juu ya udaktari wa Biblia, yaani “Doctor of Divinity” Sasa alikuwa na uhuru wazi wa kushughulikia mambo ya Biblia kuliko zamani. Hayo ndiyo aliyopenda mno. Alikuwa amejiwekea nadhiri kulihubiri kwa uthabiti neno la Mungu, wala siyo mafundisho ya mapapa. Sasa hakuwa mtawa wa kawaida tu, bali alikuwa mhubiri halali wa Injili, aliyeitwa kuwalisha kondoo wa Mungu ambao wanateseka kwa njaa na kiu ya neno la Mungu. Alitangaza kwa nguvu kwamba, wakristo lazima wapokee mafundiho kutoka kwa Biblia tu, wala si mahali pengine.TU 55.1

  Makutano yenye hamu ya neno walimkusanyikia. Habari njema za upendo wa Mwokozi, na msamaha wa dhambi unaopatikana kwa njia ya damu yake vilijaza furaha katika mioyo yao. Huko Wittenberg nuru ya Injili ilikuwa imewashwa tayari, ambayo itazidi kung'aa mpaka mwisho wa wakati.TU 55.2

  Lakini kuna mapambano baina ya kweli na kosa. Mwokozi wetu mwenyewe alisema, “Sikuja kuleta amani, ila upanga” Mathayo 10:34. Luther naye alisema badala ya kuanza matengenezo, “Mungu… ananisikuma kwenda mbele…. Natamani kustarehe; lakini nimetupwa katikati ya machafuko na fujo”TU 55.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents