Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uuzaji wa Msamaha

  Kanisa la Rumi lilifanya biashara ya neema ya Mungu. Chini ya ombi la kukusanya fedha za kujengea kanisa la Petro mtakatifu huko Rumi, vyeti vya msamaha wa dhambi vilitolewa kwa kuuzwa, kwa agizo la Papa. Kwa bei ya makosa kanisa lilijengwa ili kumwabudu Mungu. Jambo la namna hii ndilo lililochochea adui za papa wakaanzisha vita, vilivyotetemesha utawala wa Papa, na kuiondoa taji kichwani mwa papa.TU 55.4

  Tetzel, ambaye aliwekwa huko Ujerumani ili auze vyeti hivyo vya msamaha wa dhambi, alipatikana na hatia ya kudhulumu watu na kuasi sheria ya Mungu. Lakini aliwekwa kuajiri mradi wa askari wa kukodiwa na papa katika Ujerumani. Alijulikana kwa ulaghai wake wa kudanganya watu wajinga kwa hadithi za ajabu ajabu na kuwahadaa. Kama wangelipokea neno la Mungu wasingalidangayika lakini Biblia iliondolewa kwao, kwa hiyo wakabaki tu katika hali ya ushirikina.TU 55.5

  Tetzel alipokuwa akiingia mji fulani mjumbe humtangulia na kutangaza “Neema ya Mungu na ya Baba mtakatifu imewafikieni”. Basi watu humkaribisha mwenye kufuru huyu kama kwamba ndiye Mungu hasa. Tetzel akipanda mimbarani, katika kanisa husifu sana vyeti vya msamaha na kusema kuwa hivyo ndivyo karama ya Mungu ya thamani kwa wanadamu. Husema kuwa kwa njia ya vyeti hivyo dhambi zote ambazo mtu atatenda baadaye husamehewa wala hakuna haja ya kutubu. Cheti kimekamilisha mambo yote. Aliwahakikishia wasikilizaji wake kwamba cheti hicho kina uwezo wa kuokoa mtu aliyekufa; mara ile fedha inapotumbukizwa katika kisanduku. Roho ya marehemu hupita moja kwa moja bila kuingia matesoni kwanza mpaka mbinguni.TU 55.6

  Hivyo fedha na dhahabu vikamiminika katika sanduku la Tetzel. Wokovu ulipatikana kwa njia ya kuununua ulikuwa rahisi kuliko wokovu unaopatikana kwa njia ya kutubu. Imani na juhudi ya kupinga majaribu ya dhambi, mpaka upate mtu ushindi.TU 56.1

  Luther alijazwa na hofu mno. Wengi hata katika watu wake walikuwa wamenunua vyeti vya msamaha. Mara wakaanza kumjia mchungaji wakiungama dhambi huku wakitazamia kupata ondoleo la dhambi kwa njia hiyo, wala si kwa njia ya kujuta na kuziacha, wakitumaini vyeti kwamba vitawakamilisha. Luther alikataa mambo hayo na kuwaonya kuwa wasipotubu kamili na kugeuka moyo, wataagamia katika dhambi zao. Wakamwendea Tetzel wakilalamika kwamba yeye waliyekwenda kumwungamia, amekataa vyeti vyao, hata wengine wakadai warudishiwe fedha yao. Yule mtawa Tetzel akatoa matusi mazito kwa hasira nyingi, akaagiza moto uwashwe uwanjani, na akasema kuwa ameagizwa na papa kumchoma mtu yoyote atakayeupinga mpango huo mtakatifu.TU 56.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents