Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Luther Asimama Na Biblia Tu

  Wakati adui za Luther walipokuwa wakitetea mapokeo ya kibinadamu, Luther yeye aliwapinga kwa njia ya kutumia Biblia tu. Nao hawakuweza kumshinda. Kutokana na mahubiri na maandishi ya Luther, machache ya nuru ya Injili yalianza kutokea. Nuru hiyo iliwamulikia watu maelfu. Neno la Mungu lilikuwa kama upanga mkali ukatao kuwili, uliokata mioyo ya watu. Macho ya watu yalifumbwa na mapokeo ya kibinadamu kwa muda mrefu, yalifumbuliwa, wakaacha matumaini ya bure ya kuwatumaini watu ili wapate wokovu. Wakamtumaini kwa imani Kristo, Mwokozi aliyewafia.TU 58.3

  Mwamko mkuu huo uliwaogofya watawala wa kipapa. Ndipo Luther akapokea, “kuitwa shaurini” huko Rumi. Rafiki zake walifahamu hatari ya kwenda Rumi ambako kumejaa mauaji ya watakatifu. Wakamshauri asiende Rumi, ila shauri lake lisikilizwe Ujerumani.TU 58.4

  Jambo hilo lilikubalika na papa akatuma mjume ili alisikilize huko Ujerumani. Mjumbe alifahamishwa kwamba Luther amekuwa mzushi tayari. Kwa hiyo lazima ashitakiwe bila kuchelewa. Mjumbe alikabidhiwa madaraka ya kumhamisha katika Ujerumani nzima, kumtia kizuizini na kumlaani, kumpiga marufuku na kumtoa katika umoja wa kanisa. Kuwaharamisha watu wote wanaoungana naye. Kuwazuia wote katika vyeo vyote walivyonavyo kanisani na serikalini isipokuwa mfalme atakayepuuza kumkamata Luther na wafuasi wake na kuwatoa wakabidhiwe Rumi.TU 58.5

  Hakuna alama ya ukristo wa kweli iliyoonekana katika hati hiyo, wala aina yoyote ya haki. Luther hakuwa na nafasi ya kujitetea, na kuonyesha sababu ya msimamo wake. Walakini alitajwa tu kuwa ni mzushi, na kuhukumiwa pale pale.TU 59.1

  Wakati Luther alipokuwa mpweke, na kuhitaji mwenzi, Mungu alimtuma Melanchthon huko Wittenberg, ili amsaidie na kumshauri. Hali ya Melanchthon na tabia yake imara pamoja na hekima yake, vilimpatia sifa njema iliyokubaliwa na watu wote. Mara moja mtu huyo akawa mwenzi mpenzi wa Luther. Uangalifu wake, uaminifu wake na upole wake vilikuwa sifa za kumtia moyo na nguvu Luther.TU 59.2

  Huko Augsburg palikuwa pamechaguliwa kuwa mahali pa kusikiliza mambo ya Luther. Na Luther akasafiri kwa miguu kwenda huko. Vitisho vilikuwa vitolewa kwamba ataviziwa njiani na kuuawa, kwa hiyo rafiki zake walimsihi asijihatarishe kusafiri. Lakini jibu lake lilikuwa “Mimi ni mtu anayetaka kuwa mhubiri wa neno la Kristo ulimwenguni hana budi atazamie kifo wakati wowote”TU 59.3

  Habari za kwenda kwa Luther huko Augsburg ziliwafurahisha sana wajumbe wa Papa. Mtu mkorofi, anayechafua ulimwengu aonekana sasa kuwa katika uwezo wa Rumi. Hivyo hawataaweza kuepuka. Wajumbe wa papa waliazimu kumlazimisha Luther ili akane imani yake, au kama hilo halitawezekana, wamtie mikononi mwa walinzi, wampeleke Rumi ili akashiriki mambo yaliyowapata akina Huss na Jerome. Hivyo basi, mjumbe wa papa akashauri, kwa njia ya balozi, kwamba wamshawishi Luther asafiri bila mlinzi akitumaini tu bahati yake. Jambo hili lilikataliwa na Luther. Hakukubali kusafiri, mpaka apate kuhakikishwa na mfalme kuwa atamlinda kamili, ndipo atakubali kwenda kuonana na wajumbe wa papa.TU 59.4

  Basi, wajumbe wa papa walikusudia kumshawishi Luther kwa ujanja. Wakaonekana kuwa watu wa upendo mwingi kwa Luther. Wakamshauri akubali tu kushikamana na kanisa na kanuni zake bila ubishi, wala kuhojiana. Lakini jawabu la Luther lilionyesha jinsi anavyolipenda kanisa na ukweli wa Biblia. Pia kwamba yuko tayari kujibu maswali yote kuhusu mafundisho yake, na kukubali wakuu wa chuo alikofundisha watoe uamuzi wao juu ya mafundisho yake. Lakini alikanusha mambo ya maaskofu kwamba akane imani yake bila kumthibitishia kosa lake.TU 59.5

  Wao walikazana tu kusema, “Kana imani yako! Kana Imani yako”. Luther aliwaonyesha kuwa msimamo wake unatokana na maandiko matakatifu na hakuweza kukana ukweli. Mjumbe wa Papa aliposhindwa kumthibitishia Luther kosa kutokana na Biblia, basi wafuasi wa Rumi wote wakamzomea na kumtukana, wakimwita kuwa mhalifu wa mapokeo ya wazee na mzushi na kadhalika. Wala Luther hakupata nafasi yoyote ya kusema. Baadaye alipata ruhusa ya kutoka kuonyesha majibu yake kwa maandishi.TU 60.1

  Alipoandika rafiki yake, alisema, “mambo yaliyoandikwa yanaweza kutumiwa kumhukumu mtu mwingine. Pili, mtu anaweza kutatanika kwa hofu, wala si kwa dhamiri, wakati watu wanapopayuka payuka kwa majivuno na maneno mengi ya ovyo ovyo”.TU 60.2

  Wakati mwingine Luther alipofikishwa barazani, alieleza wazi msimamo wake, ukiungwa mkono na maandiko matakatifu. Alisoma maneno yake aliyoyaandika katika karatasi, baada ya kuyasoma kwa sauti wazi, akampa askofu mkuu hiyo karatasi. Askofu mkuu aliitupa kando huku akimlaani Luther na kusema ni mwingi wa maneno maovu ya kivivu yasiyohusu. Sasa Luther akakutana na askofu mwenye kiburi, akamgusa kwenye siri yake. Akagusa mafundsiho wanayofundisha kanisa, ambayo ni mapokeo matupu.TU 60.3

  Askofu akijaa na ghadhabu alipaza sauti, “Kana imani hiyo au sivyo nitakupeleka Rumi. Akarudia kusema tena Kana imani, au sivyo hutaonekana tena”.TU 60.4

  Basi Luther na rafiki zake wakaondoka huku akisema kuwa wasitazamie kuwa atakana imani. Askofu hakukusudia kuwa mambo yatakuwa hivyo. Basi wakabaki wakitazamana kwa mambo yalivyotokea, na kwamba mpango wao umeshindwa.TU 60.5

  Mkutano mkuu uliokutanika uliweza kupima kati ya watu hao wawili, roho ya aina gani waliyo nayo, na misimamo yao. Ukweli ulijidhihirisha uliko. Luther akiwa mtulivu, mwenye ukweli na imara mjumbe wa papa mwenye majivuno bila kuwa na neno lolote la Biblia lenye kumwunga mkono, huku akipiga tu kelele, “Kana imani, au sivyo nitakupeleka Rumi”.TU 60.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents