Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  8/Jasiri wa Kweli

  Mfalme mpya alikalia kiti cha ufalme wa Ujerumani, ambaye ni Charles V. mtawala Saxony ambaye Charles alikuwa akimtegemea, alimshauri asijihusishe na habari za Luther, mpaka hapo akatapopewa nafasi ya kujitetea mbele zake. Kwa mashauri hayo mfalme alitiwa katika hali ya wasiwasi. Wafuasi wa papa wasingalitosheka na kitu chochote, ila kifo cha Luther. Mfalme wa Saxony alimwambia mfalme Charles V kuwa Luther apatiwe mlinzi ili “aje afike mbele ya wataalamu na watawa na mahakimu wasiopendelea”TU 65.1

  Basi mkutano ukakutanika katika mji wa Worms. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa wakuu wa Ujerumani kukutanika pamoja na mfalme wao kijana. Viongozi wa kanisa wakuu wa serikali na mabalozi kutoka nchi mbalimbali walikutanika huko Worms. Lakini tamasha halisi iliyoutayaharukisha mkutano ilikuwa “Mtengenezaji wa kanisa” yaani Martin Luther. Mfalme Charles aliambiwa mkuu kuja pamoja na Luther, huku akimhakikishia ulinzi kamili na uhuru wa kusema bila kizuizi. Luther alimwandikia mkuu huyu hivi, “kama mfalme ndiye ameniita, siwezi kuwa na wasiwasi, maana ni kama kuitwa na Mungu mwenyewe Kama wanakusudia kunidhuru…. Najikabidi mikononi mwa Bwana… Bwana asiponiokoa maisha yangu hayana faida…. Unaweza kutazamia kila kitu kutoka kwangu... Ila huwezi kunitazamia kukimbia au kukana imani yangu. Kukimbia siwezi, na kukana imani siwezi pia.”TU 65.2

  Habari zilipoenea kwamba Luther atasimama mbele ya baraza la wakuu, wasiwasi mwingi ulienea. Alexander, ambaye ndiye mjumbe wa papa, alikasirika mno. Kuhusika katika kesi ambayo papa mwenyewe amekwisha kutoa hukumu na kumpiga mtu huyo marufuku ni jambo baya sana, linalofedhehesha mamlaka ya papa. Alimshauri Charles kutoruhusu kusimama na Luther huko Worms, na kutoruhusu akamshawishi mfalme akubali. Alexander hakutosheka na ushindi huo aliopata wa kumshawishi mfalme bali alijitahidi kusema kuwa Luther ni mwenye hatia anayestahili hukumu akimshitaki kuwa ni “Mchochezi, mwasi, mkaidi na mwenye kufuru”. Lakini harara yake ilidhihirisha aina ya roho iliyomwongoza kumshitaki. Alisukumwa tu na chuki kutaka kulipa kisasi. Hivyo ndivyo ilivyoonekana.TU 65.3

  Alexander akamsisitiza mfalme kwa bidii sana ili atekeleze amri ya papa. Aliposhindwa na mashawishi ya Alexander mfalme akamwambia kuwa alete kesi hiyo mbele za wakuu. Wale waliomwunga Luther mkono wakasikiliza usemi wa Alexander kwa wasiwasi mwingi. Mtawala wa Saxony hakuwako siku hiyo, lakini baadhi ya washauri wake waliyaandika maneno ya hotuba ya ujumbe wa papa.TU 65.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents