Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Luther Ashitakiwa Kuwa Mzushi

  Alexander alimshambulia Luther kwa usemi wa nguvu na ufasaha, kwamba ni adui wa kanisa na wa serikali pia. Akasema kuwa makosa ya Luther yametosha, na yanasababisha kuwachomelea mbali wazushi laki nzima.TU 66.1

  Kundi la wakufunzi wapotofu na wafedhulu, ambao ni makasisi walioharibika, na watawa wapumbavu, pamoja na jamii ya wa tu waovu, walisema. “Waluther hawa wana nini? Je hesabu yao inawiwa na hesabu ya Wakatoliki na uwezo wao ni kitu gani kwa uwezo wa Wakatoliki? Amri ikitolewa na watu hawa ingetekelezwa mara bila kupingwa na kitu”.TU 66.2

  Mabishano yale yale bado yanaendelea kwa wote wanaoeneza ukweli wa neno la Mungu. Kila mara maswali hutokea, “ni nani hawa wanaojidai kutangaza mafundisho mapya? Kwanza hawana elimu, ni wachache kabisa, nao ni watu duni tu. Hata hivyo wanasema kuwa wanao ukweli na kwamba wamechaguliwa na Mungu. Ni wajinga kabisa na wamedanganyika. Je, kanisa letu linalinganishwaje nao kwa umaarufu na kwa wingi?” Mashindano ya jinsi hiyo hayatofautiani na yale ya wakati wa Luther.TU 66.3

  Luther, akiwa na uwezo wa neno la Mungu ili kuwapinga na kuwaponda watetezi wa papa. Ilionekana kuwa sio mafundisho yake tu yangelaaniwa ila hata yeye angeangamizwa. Mambo yote Roma iliyokusudia kusema juu yake, yalisemwa kwa hiyo tofauti ilionekana baina ya ukweli na uwongo wakati wa mapambano ya wazi.TU 66.4

  Sasa Bwana aliwaamsha wana baraza waone wazi juu ya udhalimu wa mapapa. Duke George wa Saxon akasimama katika baraza hiyo ya wakuu akafafanua kwa ukamilifu kabisa udanganyifu wa maovu ya kanuni za papa.TU 66.5

  Dhuluma….. hupiga kelele kuhusu Roma. Aibu yote imewekwa kando, kile wanachokazania ni fedha…. Kwa hiyo wahubiri ambao wangehubiri ukweli, hawasemi lolote, ila madanganyo. Hivyo sasa wanavuna walichopanda. Kadiri mpango huo ndimo maji ya udhalimu hububujika. Upotovu unaonyesha udhalimu na tamaa ya mali mkononi….. Lo! Ni aibu inayoletwa na viongozi wa kanisa, inayowatumbukiza watu maskini katika uangamivu wa milele. Kazi ya matengenezo ya kanisa lazima ipingwe. Kwa kuwa msemaji wa papa alikuwa adui wa Luther aliwashawishi wasikilizaji ili wamwunge mkono.TU 66.6

  Malaika wa Mungu walitoa nuru katika giza nene la makosa, akafungua mioyo ya watu wauone ukweli. Uwezo wa Mungu uliwakirisha hata wapinzani wakuu ili waandae njia kwa matengenezo makuu zaidi. Sauti ya mkuu zaidi ya Luther imesikika katika baraza hilo.TU 67.1

  Kamati ikachaguliwa ili ipange mambo maovu ambayo wametendea na papa kwa watu wa Ujerumani. Orodha hio imepelekwa kwa mfalme, akiombwa ili achukue hatua kuhusu mambo haya ya udhalimu. Mtu mmoja kati ya waombaji alisema, “Ni kazi yetu kuzuia maovu na kuwaheshimu watu wetu. Kwa hiyo tunakuomba kwa unyenyekevu uamuru matengenezo ya kanisa yafanyike na kukamilishwa”.TU 67.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents